Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya Riadha ya Taifa yaliyokuwa yafanyike Julai 5 na 6 mwaka huu, jijini Arusha, yameahirishwa na tarehe mpya itatajwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania ( RT), Wilhelm Gidabuday, amesema mashindano hayo yameahirishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa shirikisho.
Anasema hata hivyo anawahakikishia wadau wote wa riadha nchini kwamba Mashindano ya Taifa yatafanyika baadae mwezi huu Arusha kwa tarehe itakayotangazwa wiki ijayo.
“Pamoja na changamoto zilizo nje ya uwezo wetu; pia itakuwa fursa kwa mikoa kutumia wachezaji waliopo katika Umetashumta kule Arusha yanayomalizika hivi karibuni,” alisema.
Pia, alisema kwa niaba ya Shirikisho la Riadha Tanzania anapenda kuujulisha umma wa Watanzania kwamba tayari wameshawasilisha majina ya wanariadha 15 BMT pamoja na taarifa zao kama walivyoagizwa na BMT kuelekea Mashindano ya Afrika (All African Games) yatakayofanyika Rabat Morocco.
Alisema RT wameanza matayarisho ya timu ya Mashindano ya Dunia itakayofanyika kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 6 mwaka huu, Doha Qatar, wanariadha watano waliofikia viwango stahiki wanatarajia kujinoa Iten Kenya (kambi ambayo inatumiwa na wanariadha nyota duniani).
Gidabuday, aliomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.
Aidha, Katibu huyo aliiomba mikoa iendelee kujiandaa na maandalizi na tarehe mpya ya mashindano itakayotangazwa hivi karibuni.
Mashindano ya taifa hushirikisha kombaini za mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

No comments:
Post a Comment