HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2019

Tusiime yatoa wito kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu hasa wasioona

Ofisa Masoko wa Shule ya Tusiime, Ndemugoba Nyagwe, akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani).  


Na Janeth Jovin

SHULE ya Sekondari ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam imewataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu wakiwemo wasioona kuwaleta katika shule hiyo kwani wameanza kutoa elimu kwa kundi hilo  kwa lengo la kuwainua  kama ilivyo kwa watoto wengine.

Aidha shule hiyo imetoa wito kwa shule mbalimbali hususani za binafsi, kujenga utaratibu wa kushiriki katika maonyesho ya 43 ya kimataifa ya biashara kwa kuwa ndio fursa pekee ya kujitangaza kitaifa na kimataifa.

Akizungumza katika viwanja vya maonyesho hayo vya Mwalimu Nyerere vilivyopo kurasini Temeke maarufu sabasaba, Mchapaji na mtafsiri wa nukta nundu Tusiime, Amina Katembo alisema wanatoa elimu kwa watoto hao wenye ulemavu kwa sababu wamegundua kuwa wanauwezo mkubwa hivyo awapaswi kutengwa.

Alisema Tusiime ni shule binafsi lakini imejitoa kuwasaidia watoto hao kwa punguzo la ada hivyo wazazi wasisite kuwaleta kwa kuhofia gharama. 

Naye Ofisa Masoko wa Tusiime Ndemugoba Nyagwe, alisema watu wengi ikiwamo sekta ya waendesha shule binafsi wamekuwa wakifikiri kwamba maonyesho ni ya makampuni makubwa pekee

Alisema wao kama Tusiime ni mara ya kwanza kushiriki katika maonyesho hayo, lakini wamejifunza mambo mengi na kwamba wanaamini endapo wangegundua jambo hilo mapema wangekuwa wamefika mbali.

"Hili wazo la kushiriki katika maonyesho tumelipata mwaka huu na katika siku hizi za awali tu tumebaini kwamba hii ni fursa nzuri sana kwa ajili ya kujitangaza na kujifunza fursa mbalimbali na tunaamini tungeanza siku nyingi, tungekuwa mbali sana," alisema Nyagwe na kuongeza:

"Tatizo watu wengi wanajua kwamba kushiriki katika maonyesho haya ni mpaka uwe na kiwanda au kampuni kubwa,  naomba wafahamu kwamba hapa ndio mahali pazuri pa kuanzia, kujitangaza na kujifunza pia"

Alisema kama kaulimbiu ya maonyesho hayo inavyosema kwamba uchumi wa viwanda na usindikaji wa bidhaa za kilimo, wao kama tusiime wanaunga mkono kaulimbiu hiyo na tayari wamejipanga mbali na kufundisha masomo yaliyozoeleka kwa wanafunzi wao, lakini pia kuwajengea uwezo wanafunzi wao stadi za kazi na maisha

Alisema Tusiime kwa kuanza tayari wanaprogramu mbalimbali kwa upande wa kundi maalum la watu wenye ulemavu kuwajengea uwezo katika kazi mbalimbali za mikono.

No comments:

Post a Comment

Pages