HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2019

Wananchi watakiwa kujiunga na Bima

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Oyuke Phostine, akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani. Katika viwanja vya sabasaba.

 
Na Janeth Jovin

MAMLAKA ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA) imewataka watanzania kuhakikisha wanajiunga na huduma za bima kwa ajili ya kuwakinga na majanga mbalimbali pamoja na usalama wa mali zao.

Aidha Mamlaka hiyo imesema zaidi ya kampuni 30 za bima zimeshiriki katika maonyesho ya 43 ya kimataifa ya biashara  yayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa mtu kuwa na bima maishani.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika Viwanja vya maonyesho hayo vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano wa TIRA, Oyuke Phostine alisema kuwa dhumuni la kushiriki katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kujiunga na bima.

Alisema pia watahakikisha wanaangalia mifumo ya utoaji wa bima imaimarika nchini na elimu hiyo kwa wananchi inaendelea kutolewa kwa wingi.

“Tunatambua kuwa mtu akipata elimu hii ya umuhimu wa bima inakuwa rahisi kwake kujiunga hivyo TIRA tutaendelea kuyasimamia makampuni haya ili yatoe elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa bima, lakini pamoja na utoaji wa elimu mamlaka katika maonyesho haya tutaangalia mifumo ya utoaji wa bima inaimarika,” alisema Phostine.

Aidha alisema katika maonesho ya mwaka jana awakuboresha vitu vingi kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kushiriki lakini kwa mwaka huu wameboresha na wamefanikiwa kuingia katika ushindani.

No comments:

Post a Comment

Pages