Na Tatu Mohamed
WASANII wakongwe kwenye tasnia ya muziki ambao ni ndugu
wa familia moja Unique Sisters, wameibukia katika Maonyesho ya 43 ya
Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) katika banda la kampuni ya uuzaji wa
vipuri vya mashine na vyombo vya moto ya Saint Parts.
Akizungumza
katika maonyesho hayo, mmoja wa wasanii hao, Radhia Kipozi amesema
wamekuwa kimya kwa muda mrefu sababu ya kutokuwepo nchini.
Amesema
kutokana na sera ya Tanzania ya viwanda mbali na masuala ya muziki
wameamua kuingia katika kampuni ya kijapani na kuwatangazia biashara zao
kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa na maendeleo zaidi.
"Nilikuwa
Japani hawa watu wa Kampuni ya Saint Parts ambao ni wauzaji wa mafuta
ya vyombo vya moto na vipuri wa nchini Japani wamenileta hapa ili kuja
kuwa mkarimani wao katika maonyesho hayo.
"Mwaka
2017 tulitoa singo ijulikanayo kwa jina la kwako ambayo ipo katika
youtube na sasa hivi tunatarajia kuja na ujio mpya wa kazi ambayo
tunaamini itaturudisha katika Game ya mziki," amesema.
Aidha
amesema mashabiki wao wakae mkao wa kula kwa kupata kitu kizuri ambacho
kitawatambulisha tena katika nyaja ya mziki huku wakihakikisha
wanatumia bidhaa ambazo wamekuja kuzitambulisha kutoka Japani.
No comments:
Post a Comment