HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2019

VETA yawataka watanzania kupenda bidhaa za ndani

Na Janeth Jovin

MAMLAKA ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imewataka watanzania kuhakikisha wanapenda  zaidi bidhaa za Kitanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika maonyesho ya 43 ya kimataifa sabasaba, Mwalimu wa
VETA Immanuel Bukuku alisema kuna umuhimu mkubwa kwa watanzania kupenda bidhaa za ndani zaidi.

Alisema kwa mwaka huu VETA imeleta mashine ya kuoka aina mbalimbali ya nyama ikiwemo ndafu, nyama ya kuku na  ng'ombe ambayo utumia mfumo wa gesi na umeme.

Bukuku alisema mashine hiyo inauwezo wa kuoka kuku zaidi ya watano  na nyama ya ng'ombe kwa muda mchache zaidi tofauti na ndafu uchukua masaa sita kuiva.

"Tumeleta mashine hii katika sabasaba ya mwaka huu ili watanzania waweze kuona jinsi  ya kuoka ndafu na nyama ya kawaida, hii ni mashine ambayo ni  automatic na joto lake  ni la kuchagua kulingana na kitu unachokioka," alisema

Alisema mashine hiyo ni rahisi kutumiwa na urahisisha nyama kuiva kwa wakati
Kulingana na muda wanayoweka katika mashine hiyo.

"Mashine hii katika kuoka ndafu inatumia umeme kiloweti 5 ambapo kuna tempreture contro inayohakikisha umeme unaokea nyama hiyo  ambpo inauwezo wa kutumia mfumo wa gesi," alisema

No comments:

Post a Comment

Pages