Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wake na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike (katikati), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema mashindano ya kombe
la mataifa barani Afrika mwaka 2019 yanayoendelea kufanyika nchini Misri,
yamebeba uzito wa kipekee kwa nchi ya Tanzania baada ya kukaa nje kwa miaka
thelathini na tisa (39) na kufuzu kushiriki katika mashindano hayo ambayo Timu
ya Taifa ya Tanzania imetupwa nje katika hatua ya makundi baada ya kupambana na timu za Senegal,
Algeria na Kenya.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari tarehe 6 Julai, 2019 baada ya
kukutana na kufanya mazungumzo na kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) Raia wa Nigeria Emmanuel Amunike katika hotel ya Protea Courtyard Jijini
Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa bado ana imani kubwa na Kocha huyo kuendelea
kufanya vizuri, kinachohitajika ni swala la muda tu, kwani amemueleza mipango
mikubwa ya kiufundi aliyonayo kwa Timu ya Taifa hili iweze kufanya vizuri
katika mashindano yajayo.
“Ndugu waandishi wa Habari kwanza
kabisa niseme tu kwamba, nimefurahi sana kukutana na kocha Mkuu wa Timu ya
Taifa ya Tanzania, ambapo lengo la kukutana naye ni kunieleza kilichotokea kule
nchini Misri katika mashindano ya Afcon ambayo tumeshiriki baada ya miaka 39
kupita, mashindano haya yamebeba uzito wa kipekee kwa nchi yetu, na niseme tu
kwamba nina imani kubwa sana na kocha Amunike kuendelea kufanya vizuri na yetu,
nimeongea naye mambo mengi sana kuhusu mashindano, na tumeona kama Wizara tumpe
muda zaidi kwa mipango mizuri ya kiufundi aliyonayo kwa Timu ya Taifa hili
iweze kufanya vizuri katika mashindano yajayo,”.
“mimi nimefurahi sana kukaa na
mwalimu, na yeye pia amefurahi kukaa na Serikali, ili tujuwe mwenzetu maoni
yake ni nini kuhusu timu ya Taifa, tufanyaje kujipanga hili kesho, kesho kutwa turejee
tena Afcon lakini safari hii tukirejea kila mtu awe na wasiwasi kuwa hii sio
timu nzuri kukutana nayo,ametupa mfano mzuri sana, kwamba Uganda mwaka 2015
iliposhiriki mara mwisho haikufanya vizuri hata kidogo, lakini wenzetu wakarudi
wakaanza kuyafanyia kazi mapungufu katika mchezo wao, badala ya kukaa mwaka
mzima mnalumbana na kunyoosheana vidole, mapungufu kwenye timu ya kiufundi na
sisi kwa upande wetu yamejitokeza sana, mengi sitayasema kwa sababu ni mambo
ambayo tutakaa na vyombo vinavyohusika, lakini cha msingi tunafurahi sana
mwalimu ana moyo chanya kwamba tunaweza, tumeonyesha watanzania kwamba
tunaweza, lakini kiufundi inatakiwa na sisi tujiongeze,” alisema Mheshimiwa
Mwakyembe.
Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amesema
Kocha Amunike amependekeza mazoezi zaidi kwa wachezaji wa Timu ya Taifa pamoja
na kucheza mechi za kirafiki kimataifa mara Tatu kwa Mwaka hili kuweza kupata
uzoefu zaidi katika mashindano ya kimataifa.
“tatizo lililojitokeza ambalo
mwalimu anadhani linaweza kutatuliwa ni mazoezi kwa timu ya Taifa,kwamba
angalau mara tatu timu ya Taifa kila mwaka ikawa na mechi za kirafiki, wanaitwa
leo wanacheza na Zambia , na Afrika Kusini, tumewakaribisha pengine Spain
wanakuja na kuangalia mbuga za wanyama, tunajenga imani ya wachezaji wetu,
kwenye mashindano haya yaliyopita tumeona kuna wakati wachezaji wetu walikosa
kujiamini, unaona mchezo kadri unavyoendelea ndio sasa hata pasi za uwakika
ndio zinapigwa, kwa hiyo ni kujiamini lakini vijana wa Tanzania walicheza
vizuri sanaa,” alisema Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment