Mhandisi Mshauri Dkt. Yonah Zaipuna akitoa ufafanuzi kwenye warsha ya
“The Power of talent.” ya siku moja iliyolenga kuwafanya vijana waweze
kuzijua na kuzitumia talanta zao katika kujikwamua kiuchumi
iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu
WAZAZI
nchini wametakiwa kulea vipaji vya watoto wao kama sehemu ya
kuwajengea uwezo na maarifa yatakayowawezesha kujiajiri na hatimaye
kutoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam baada ya warsha ya kueleza
nguvu ya vipaji au talanta (The Power of Talent), Mwanasheria na Mtunzi
wa Mashairi, Aisha Kingu, amesema wazazi au walezi wana nafasi kubwa ya
kukuza talanta za watoto wao.
“Nimeandaa
warsha hii ili kwa pamoja tujadili namna nzuri ya kutambua na
kuendeleza vipaji vya vijana ili viwe nyenzo muhimu katika kujiinua
kiuchumi,” almesema na kuongeza: “Hayo yote yanawezekana iwapo tu wazazi
na walezi wataamua kwa dhati kuunga mkono talanta za vijana na
kuwafanya watimize ndoto zao za kimaisha.”
Mmoja
washiriki, Dk. Kingu Mtemi, ametoa ushuhuda wa wazazi kuendeleza
talanta za watoto na kufafanua taabu inayoambatana na ulezi wa aina.
“Sisi wazazi mwanzoni tulikuwa na wakati mgumu kwani tuliamini binti
yetu angekuwa daktari. Lakini kadiri muda ulivyoenda tulizoea hali hiyo
na kuamua kuunga mkono kipaji chake cha uandishi wa mashairi ambacho
alikionyesha tangu hatua za awali ya masomo yake,” alisema Dk. Mtemi
Aisha
ni mtoto wa Dk Mtemi. Bw Mtemi ameeleza kuwa baada ya kumwacha Aisha
ajikite katika fani aipendayo alifanikiwa baada ya muda mfupi tu.
“Kwa
kipindi kifupi binti huyu amepata mafanikio makubwa ikiwemo kuwaandikia
mashairi viongozi wa ndani ya nchi akiwemo Rais mstaafu Jakaya Mrisho
Kikwete. Lakini pia safari yake ya mashairi imemkutanisha na Rais Putin
wa Urusi, Malikia Elizabeth wa Uingereza pamoja na watu maarufu mbali
mbali duniani,” alisema
Dk
Mtemi ameshauri wazazi na walezi wajitahidi kugundua na kuendeleza
talanta za watoto na kusisitiza kuwa watoto wawe huru kufanya
wanavyovipenda na kuepuka kuwalazimisha watoto kuingia katika fani
wanazozipenda na wazazi au walezi.
Elham Mwema amepongeza waandaji wa warsha ili wazazi waelewe umuhimu wa kugundua na kuendeleza talanta watoto wao.
“Warsha
imekuwa nzuri na imetufanya vijana tuone nguvu za vipaji na kutambua
njia za kuendeleza vipaji . Tumeona kwamba kipaji kikiendelezwa ni
rahisi kufanikiwa kiuchumi na maana mafanikio yanatokana na kufanya
kitu ambacho kwako unakifurahia,” alisema Mwema.
No comments:
Post a Comment