HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 26, 2019

Diamond awa balozi wa sabuni, awashauri Vijana wenzake kutokata tamaa

NA JANETH JOVIN

MSANII Nassib Abdul ‘Dimond Plantinum’ amewataka vijana waliopo nchini  hasa wasanii wenzake kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa ili waweze kutimiza ndoto zao.

Diamond aliyasema hayo leo katika hafla ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuwa balozi wa Kampuni  Bomet  kupitia sabuni yao ya unga ya Niceone.

Msanii huyo ambaye alifika eneo la tukio akiwa na ulinzi mkali wa walinzi 11 waliovalia mavazi meusi na miwani meusi, alisema siri pekee ya mafanikio yake ni namna anavyojituma na kutokana tamaa katika kila jambo analolifanya.

Alisema anayafanya hayo yote akibebwa na historia ya maisha yake ya nyuma ambayo yalijaa dhiki lakini hakukata tamaa na aliamini siku moja ndoto yake itafanikiwa.

“Mimi wakati natafuta fedha nilifanya kazi mbalimbali ikiwamo kuuza mitumba, kupiga picha, na hata nilipoingia kwenye muziki nilijituma sana  nikiamini siku moja nitatoka,”alisema na kuongeza

“Mimi niwashauri vijana wenzangu tujitume kwelikweli bila kukata tamaa, kazi yoyote unayoiyona  itakuingizia kipato basi ifanye kwa bidii na uaminifu, lakini kikubwa tusiache kumuomba Mungu, naamini kila mmoja akifanya hivyo atafanikiwa maana Mungu kampa kila mtu fungu lake,”alisema

Aidha alisema pamoja na kujituma ni muhimu kijana kuwa mwaminifu na mwadilifu katika kulinda na kutunza ushuhuda wao machoni pa watu na kuwa waaminifu mbele za Mungu kwa kurudisha shukrani kwa jamii hususani watoto yatima, wazee na wasiojiweza.

Naye Ofisa Masoko wa sabuni ya Niceone Anna Semtumbi alisema mbali na Diamond kutangaza bidhaa ya kampuni yao, pia watafanya shughuli mbalimbali za kijamii kwa lengo la kurudisha shukrani zao.

Alisema Diamond atakuwa barozi wa sabuni hiyo ambayo inakusudia kuleta unadhifu na kuwaunganisha watanzania popote pale walipo pasipo kujali wasifu wao.

No comments:

Post a Comment

Pages