Na Alodia Dominick, Bukoba
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ruhaga Mpina, ameitaka Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera kutoza ushuru wa kilo ya samaki kwa wavuvi kwa kiwango cha shilingi 100.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ruhaga Mpina, ameitaka Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera kutoza ushuru wa kilo ya samaki kwa wavuvi kwa kiwango cha shilingi 100.
Waziri Mpina alitoa agizo hilo jana wakati umoja wa vijana wa CCM walipokuwa kwenye maadhimisho ya Bukoba ya Kijani yaliyofanyika katika Kata ya Kemondo mkoani hapa baada ya mbunge wa vijana Halima Bulembo kupokea kero kutoka kwa wakazi wa Kemondo kuhusiana na wavuvi kutozwa shilingi 200 kwa kilo ya samaki, ndipo alimpigia simu waziri huyo na kujibu kero hiyo.
Mpina alisema, wizara imetoa maagizo ya kuzitaka halmashauri zote kutoza kiwango kimoja wasipofanya hivyo sheria itarekebishwa na tozo ya samaki kilo itarudi shilingi 100 na kuwa halmashauri ya Bukoba na Ukelewe zimekuwa zikiwachanganya wananchi kwa kutoza viwango tofauti na halmashauri nyingine.
Kwa upande wa mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo alieleza kwamba, mkoa ulianzisha kampeini ya Kagera ya kijani ili kuhamasisha kijani pamoja na kueleza utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm kutoka kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jonh pombe Magufuri ambayo iliazimishwa kimkoa na sasa inaazimishwa kila wilaya za mkoa huo.
Wakati huo huo, katika maadhimisho hayo vijana zaidi ya 15 kutoka chama cha democrasia na maendeleo Chadema kata ya kemondo akiwemo mwenyekiti wa kitongoji cha Kigarama wamekabidhi kadi zao na kujiunga na CCM.
Mmoja wa vijana hao Bushira Hamidu alisema, kilichomshawishi kurudi ccm ni baada ya viongozi wa chama hicho kuahidi kutatua kero ya ardhi ya mlima wa Katwenkoko ardhi iliyokuwa imechukuliwa na viongozi wachache.
"Kama kuna kiongozi yeyote alishiriki katika kudhurumu ardhi ya wananchi lazima chama kimchukulie hatua katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kumuweka kando kiongozi kama huyo" Alisema mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Bukoba vijijini Evarista Babyegeya.
No comments:
Post a Comment