HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 22, 2019

GETRUDE MONGELA MGENI RASMI TAMASHA LA 14 LA JINSIA

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi.


NA TATU MOHAMED

BALOZI Getrude Mongela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho katika ufunguzi wa Tamasha la 14 la Jinsia linatakalofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), Mabibo jijini Dar es Salaam.

Tamasha la 14 la Jinsia litafanyika kuanzia Septemba 24 hadi 27 mwaka huu na limeandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wanawake na usawa wa kijinsia pamoja na wanaharakati binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi, alisema zaidi ya watu 1000 watashiriki katika tamasha hilo wakiwemo wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi mbalimbali kutoka halmashauri na serikali juu, wanaharakati ngazi mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

Aliongeza kuwa wageni kutakuwa na wageni kutoka Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Swaziland, Kenya, Uganda, Ghana na Zimbabwe.

“Kipekee Tanzania itakumbukwa katika historia ya kuweka misingi ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake kwani katika mkutano wa Beijing balozi Gedrude Mongela aliibuka kidedea kuwa Katibu Mkuu wa mkutano huo wa kihistoria.

" Hatua hiyo iliinua Nchi katika ramani ya dunia, katika kuendelea kuenzi na kuthamini mchango wa Mongela TGNP na tapo la ukombozi tumeamua kumchagua Mongela kuwa mgeni rasmi katika tamasha la mwaka huu," alisema Liundi.

Alibainisha kuwa tamasha la Jinsia mwaka huu lina umuhimu wa kipekee kwani kitaifa na kidunia wameanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya azimio la mpango kazi wa Beijing, ambapo kilele chake ni mwaka 2020.

Alisema kuwa maandalizi ya Mkutano wa Beijing yalikuwa chachu kubwa ya kuanzishwa na kuimarishwa kwa asasi nyingi zinazotetea haki za wanawake nchini.

“TGNP Mtandao ni mojawapo ya asasi iliyoleta chachu kubwa ya kuunganisha wadau mbalimbali kutoka vikundi vya wanawake , wanazuoni na mitandao ya wanawake kupata Sauti ya pamoja katika ushiriki wa mkutano wa Beijing.

“Kwa mantiki hiyo TGNP Mtandao inaendelea kusherehekea uwepo wake kwa zaidi ya miaka 25 sambamba na maadhimisho ya Mkutano wa Beijing,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages