HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 05, 2019

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA RELI CHATOA ELIMU KWA ABIRIA WANAOTUMIA USAFIRI HUO

Jeshi la Polisi kupitia kikosi chake cha Reli leo kimetoa Elimu kwa Abiria wanaotumia usafiri wa Treni juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na uhalifu unaofanywa na baadhi wa matapeli, elimu hiyo imetolewa na SGT Michael, eneo la kamata kariakoo jijini Dar es Salaam mapema leo kabla abiria hao kuanza safari ya kuelekea Mkoani Kigoma. 
Huku akisema kwa kipindi kifupi ambacho safiri za treni zilisimama baadhi ya watu walitumia nafasi hiyo kama sehemu ya kujipatia kipato kwa kuwatapeli abiria kwa njia ya kukatisha tiketi feki.
 
Aidha katika hatua nyingine SGT Michael aliwataka wanandoa pamoja na watu wengine wanaotumia usafiri huo kuacha kuwafanyia ukatili wa kijinsia wenza wao au watoto wao huku akisema kuna baadhi watu husafirisha familia zao hasa kwa wanawake wajawazito ambao wamekaribia kujifungua hali hiyo huwapelekea wanawake hao kujifungulia ndani ya Treni.

No comments:

Post a Comment

Pages