HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2019

KASHASHA ATETEA KITI CHA UENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA

Deogratias Kashasha akipiga kura.
 Wagombea wakiwa katika picha ya pamoja.
 Rwekaza Deusdedit


Diwani wa Kishanje wilayani Bukoba mkoani Kagera Bwana Deogratias Kashasha amefanikiwa kutetea kiti cha Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Uchaguzi huo umefanyika Septemba 5 mwaka huu katika kikao cha baraza la madiwani kwa ajili ya kufunga mwaka 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Awali mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Hashim Murshid Ngeze amesema wazi majina ya wajumbe walioomba nafasi ya kugombea nafasi hiyo na kuwataja wagombea ambao ni Bwana Deogratias Kashasha ambaye ni Diwani wa kata ya Kishanje kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM na Rwekaza Deusdedit diwani wa kata ya Katoma kupitia chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema.

Kabla ya uchaguzi huo Mwenyekiti huyo amevitaja vyama vilivyopendekezwa katika kugombea nafasi hiyo kuwa ni CCM, CUF, CHADEMA ambapo vyama viwili chama cha mapinduzi CCM na chama cha Democrasia na maendeleo Chadema ndivyo vilivyojitokeza na kupatikana kwa wagombea hao.

Jumla ya wapiga kura ni 35
Ambapo Bwana Deogaratias Kashasha kuibuka kwa kura 28 dhidi ya Mpinzani wake Rwekaza Deusdedit wa Chadema aliyeibuka na kura 7.

Aidha Bwana Kashasha ametangazwa kuwa mshindi kwa kuchukua nafasi ya makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani hapa.

Bwana Kashasha ametoa shukrani zake za dhati kwa madiwani hao kwa kumchagua kutetea kiti hicho na kuahidi kufanya kazi kwa matakwa ili kutekekeza ilani ya chama cha mapinduzi CCM.

No comments:

Post a Comment

Pages