HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2019

1,600 kushiriki kongamano la biashara leo

NA SULEIMAN MSUYA

WATU 1683 wamejisajili kushiriki Kongamano la Kwanza la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na nchi ya Uganda.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa  habari jana jijini Dar es Salaam.

Waziri Bashungw alisema kongamano hilo litakalofunguliwa na Rais John Magufuli na Yoweri Museven wa Uganda kitajikita katika kujadiliana namna ya nchi zao kufanya biashara.

Alisema pia watajadili Sera na Sheria zilizopo ili kuhakikisha haziwi vikwazo vya kibiashara katika nchi zao.

"Zaidi ya washiriki 1,600 wamethibitisha kushiriki kongamano la kwanza la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uganda ni matumaini yangu litakuwa na tija kwa pande zote," alisema.

Waziri Bashungwa alisema katika kongamano hilo wafanyabiashara wazawa zaidi 1,000 na Waganda zaidi ya 400 watashiriki kujadili biashara zao.

Waziri alisema ni matumaini yake washiriki watatoka na lugha moja ambayo itachochea ukuaji wa uchumi kwa nchi zao.

Alisema Tanzania inafanya bias had a na Uganda katika bidhaa za kilimo na vifaa vya viwandani.

Bashungwa alisema Tanzania inataka kutumia nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC), ili kuifanya Tanzania kuwa eneo la uzalishaji bidhaa muhimu kwa kila nchi.

Alisema mkakati wa kuondoa vikwazo vya biashara unaendana na kujenga ushirikiano mzuri na nchi jirani na ndio wameenza na Uganda.

Alisema iwapo biashara zitakuwa katika ukanda wa EAC na SADC ni dhahiri kuwa lengo la Tanzania ya viwnada litatimia.

No comments:

Post a Comment

Pages