HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 30, 2019

Maelfu Dar wajionea gulio la Voda M-pesa

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji, Mrakibu Mwandamizi Al-Hajj Ally Mtanda (kushoto), akitoa maelezo kuhusiana na Huduma za Idara ya Uhamiaji kwa Mkurugenzi wa M-pesa Vodacom Tanzania PLC, Epimack Mbeteni, kwenye gulio la M-Pesa (M-Pesa Expo) jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande).

 
 NA MWANDISHI WETU 

KAMPUNI kinara wa mawasiliano ya simu Tanzania, Vodacom Tanzania PLC, jana  ilizindua huduma yake ya LIPA KWA SIMU katika gulio la M-pesa lililofanyika Mlimani City Mall, jijini Dar es Salaam. 

Malengo ya gulio hilo ni kuongeza ufahamu wa upana wa huduma za kifedha zinazotolewa na mfumo wake mpya wa malipo. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni, alisema Vodacom Tanzania imeanzisha njia hiyo kwa kuona hitaji la kupanua mfumo wa LIPA kwa M-Pesa kutoka katika mfumo wa M-Pesa.

Alisema moja ya manufaa ya mfumo huo ni pamoja na kuweza kupokea malipo kutoka mitandao na benki zote na kufikia katika kuwezesha malipo ya kidijitali katika mifumo ya rejareja na manunuzi mitandaoni. 

Alisema, Vodacom imezindua huduma hiyo ya "Lipa Kwa Simu" kuhamasisha matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali kama njia kuu ya malipo nchini na kuhama kutoka katika utegemezi mkubwa wa fedha taslimu uliopo sasa. 

"Lipa kwa Simu ni hatua ya kimapinduzi iliyochukuliwa na kampuni ya Vodacom kuelekea katika kujenga jamii isiyotumia fedha taslimu kwa kusaidia ushirikiano wa malipo katika mitandao na benki zote. 

“Kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu, wafanyabiashara na wamiliki wa biashara wanaweza kupokea malipo kutoka katika mitandao na benki zote na kuongeza ufanisi na usalama katika biashara zao.  

“Kwa upande wa wateja, bila kujali unatumia mtandao gani, sasa unaweza kufanya malipo kupitia mfumo wa LIPA kwa kutumia gharama za kawaida za kuhamisha fedha, hivyo kuepuka kutembea na kikubwa cha fedha taslimu," alisema Mbeteni.

Vodacom imewezesha LIPA kwa Simu kwa makundi ya wafanyabiashara wa sekta zote kama Baa, Hoteli, migahawa, Supamaketi, Vituo vya mafuta, kumbi za sinema, maduka ya dawa, Maduka ya vifaa vya ujenzi na kadhalika kwahivyo inapatikana kote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo ameipongeza huduma hii inayotolewa na M-Pesa na kusema imerahisisha na kuleta ufanisi katika mifumo ya malipo ya Umma.

Alisema kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kulipia bili, tozo na huduma nyingi za kijamii kupitia mfumo huu wakiwa sehemu yeyote ile, iwe nyumbani au maeneo yao ya kazi. 

No comments:

Post a Comment

Pages