HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 30, 2019

KIKEKE ATEULIWA KUWA BALOZI WA SIMBA SC KATIKA JIJI LA LONDON

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ (kushoto), akimkabidhi jezi mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Salim Kikeke, mara baada ya kuteuliwa kuwa Balozi wa klabu hiyo katika Jiji la London. (Picha na Tovuti ya Simba).
 

NA MWANDISHI WETU

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Simba SC, wamezidi kujitanua kimataifa kiutawala baada ya kufungua ‘ubalozi’ wake London nchini Uingereza.

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, jana ilitangaza kumteua Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Salim Kikeke, kuwa Balozi wa klabu hiyo katika Jiji la London, Uingereza.

Baada ya uteuzi huo, Mkurugenzi wa bodi, Mohamed Dewji ‘Mo’, alimkabidhi Kikeke jezi, ikiwa ni ishara ya makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo, ni moja ya mikakati ya Simba SC kupanua wigo wa ushindani barani Afrika na kufanana na klabu nyingine kubwa kimaendeleo.


Simba tangu imebadili Katiba na kujiendesha katika mfumo wa kampuni, imejipanga kuifanya timu hiyo kuwa ya kimataifa zaidi, kuanzia timu ya wachezaji uwanjani na kujitanua katika maendeleo mengine.

Mkataba wa Simba na Mwekezaji Mo, utagharimu Sh. Bilioni 20, ambazo zitafanikisha kupatikana kikosi bora na chenye ushindani barani Afrika, mishahara kwa wachezaji, benchi la ufundi na mengineyo.

Hivi karibuni, Mo alieleza kwamba, mwishoni mwa mwezi huu Simba inatarajiwa kuanza kuutumia uwanja wake mpya ulioko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Alisema taratibu zote za ujenzi wa uwanja huo wa mazoezi zimekamilika, kilichobaki ni kuanzia mwezi huu wataanza kuutumia uwanja wao wa Bunju.


 Alisema wanatarajia kuanza kuutumia uwanja wa Bunju mwishoni mwa Oktoba, hivyo mashabiki na wapenzi wa Simba wajiandae kupata burudani katika uwanja wao.

No comments:

Post a Comment

Pages