HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 09, 2019

TANZANIA YAITOA BURUNDI KIBABE MICHUANO YA KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2022

 Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Shaban Chilunda, akiwania mpira huku golikipa wa Burundi, Ndikumana Justin, akijaribu kuokoa katika mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.(Picha na Francis Dande).
Beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Gadiel Michael, akichuana na beki wa Burundi, Diamant Ramazani.
 Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, akiwatoka wachezaji wa Burundi katika mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Golikipa wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Juma Kaseja, (kushoto), akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kumalizika kwa mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022.
Golikipa wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Juma Kaseja, (kushoto), akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kumalizika kwa mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022.
Furaha tupu.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, wakiwa wamembeba juu kipa wa timu hiyo, Juma Kaseja.
 Kaseja akiwa juu.
 Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Juma Kaseja, akipangua penalt ya kwanza katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Said Powa).
 Golikipa wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Juma Kaseja, akiwa amebebwa juu na wachezaji wenzake baada ya kumalizika kwa mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Said Powa).
 Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, wakisangilia baada ya kuitoa burundi kwa mikwaju ya penalt katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Said Powa).

No comments:

Post a Comment

Pages