HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 25, 2019

NMB YATENGA BILIONI 1 KUSAIDIA JAMII

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la walimu.


Na Alodia Dominick, Bukoba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Generali Marco Elisha Gaguti  ameitaka benki ya NMB mkoani Kagera kuwapunguzia riba walimu kufuatia kuwa wadau wakubwa wa benki hiyo kwa muda mrefu.
 
Mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Gaguti ametoa kauli hiyo  Desemba  24 mwaka huu wakati akifungua kongamano la Walimu na Benki ya NMB lililofanyika katika ukumbi wa Elct Hotel uliopo Manispaa ya Bukoba Mkoani hapa.

Mhe. Gaguti amesema kuwa Benki hiyo inapaswa kuangalia na kuona umuhimu mkubwa kwa walimu hao kwa kuwapunguzia riba kufuatia kuwa wadau wakubwa wa taasisi hiyo kwa kipindi kirefu .

Amesema kuwa kutokana na walimu hao kuipa kipaumbele benki hiyo katika huduma hiyo kwa muda mrefu benki hiyo haina budi kuweka unafuu kwa walimu hao.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka walimu hao kuhakikisha wanatanua wigo kwa kuunda vikundi vya pamoja katika Kata zao na kuomba mikopo ya miradi mikubwa na ya pamoja ili kuinua vipato vyao hasa pale wanapostaafu.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewahimiza walimu hao kuwa mabarozi wazuri katika kuchangia kodi na kuhimiza wananchi kudai risiti pale wanaponunua bidhaa ya aina yotote jambo litakalosaidia kuongeza pato la nchi.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Gabulanga iliyopo wilayani Missenyi mkoani hapa Mutalemwa Makwabe kwa niaba ya Walimu wenzake amesema, wanaishukuru benki hiyo kwa namna inavyoendelea kuwajali walimu pamoja na kutoa misaada mbalimbali katika shule huku akidai kuwa shule yake iliwahi kupatiwa misaada mbali mbali na benki hiyo ikiweno madawati na mbao.

Naye Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Ziwa, Ibrahimu Agustino, ameeeleza kuwa, benki hiyo inatenga 1% kila mwaka katika kuihudumia jamii  na kuongeza kuwa ndani ya mwaka huu tayari zimetengwa shilingi bilioni moja ambapo hadi  sasa wametoa zaidi ya milioni mia sita katika  kusaidia jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages