Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, akiwahutubia wakazi
wa Kata ya Tambukareli katika Manispaa ya Tabora jana wakati wa kampeni
ya kufichua wahalifu katka maeneo mbalimbali mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (mwenye Tshirt nyeupe), akibadilishana
mawazo na wakazi wa Kata ya Tambukareli katika Manispaa ya Tabora jana
wakati wa kampeni ya kufichua wahalifu katka maeneo mbalimbali mkoani
humo. (Picha na Tiganya Vincent).
NA TIGANYA
VINCENT
SERIKALI ya
Mkoa wa Tabora amewataka Wenyeveti wa mitaa na vitongoji kuwa na Daftari la
Wakazi wa maeneo yao ili kuwa na orodha ya wakazi wote kwa ajili ya kudhibiti
wageni wasio waaminifu kujificha kwenye mitaa yao.
Kauli hiyo
imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri wakati wa kampeni yake ya fukua fukua inayolenga kufichua
watu ambao wanaendesha vitendo vya uhalifu kama vile ujambazi, wizi na matumizi
ya dawa za kulevya.
Alisema kuwa hatua hiyo itadumisha ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali mkoani Tabora na kuepusha wahalifu kutoka maeneo mengine kukimbilia mkoani humo.
Mwanri
aliwaonya wakazi wa Mkoa wa Tabora kutopokea wageni bila kutoa taarifa zinazowahusu
kwa viongozi wa mitaa au vitongoji vyao ili kupokea vitendo vya kuhifadhi
wahalifu.
“Endapo tutakugundua
mkazi kuishi na mgeni bila kutoa taarifa kwa viongozi wa Mtaa tutamchukulia kama
mhalifu…ni vema ukipata mgeni useme nina mgeni ameingia leo na anatarajia kukaa
katika eneo hilo kwa kipindi gani na ametokea wapi? alisema.
Mwanri
alisema uhalifu unaotoea umesababishwa na baadhi ya wenyeji kuwapokea wageni
wasio waaminifu na kuwaficha katika nyumba zao hata bila viongozi mtaani kwake
kutojua.
Katika hatua
nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora amepiga marufuku uchezaji wa michezo kama vile
bao, karata, na unywaji wa pombe za
asubuhi na muda usioruhusiwa.
Alisema
michezo yote itaanza kuchenzwa mchana ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki
kazi za uzalishaji mali na kufanyakazi za kujiingizia kipato.
Mwanri
alisema kwa upande wa vilabu vya pombe vitaruhusiwa kuuza pombe kuanzia saa
9.30 hadi saa 4.30 usiku kwa siku za kawaida na wikendi na sikukuu watauza hadi
saa 6.00 usiku.
Alisema lengo
la zuio hilo ni kuepusha baadhi ya watu kutumia maeneo hayo kama sehemu ya
kupanga uhalifu na kugeuza maficho ya wahalifu.
No comments:
Post a Comment