Kamanda wa Polisi, ACP Juma Bwire, akizungumza na waandishi wa habari.
Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi
Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi
JESHI
la Polisi Mkoa wa Iringa limewaonya wananchi wa Mkoa huo kuchukua
tahadhari wanapotumia barabara hususani kipindi hiki cha Maonyesho ya
Utalii Kusini.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi, ACP Juma Bwire alisema
wakazi wengi wamekuwa wakitumia bararabara bila kufuata tahadhari hali
inayoweza kusababisha kugongwa na magari.
" niwape
tahadhari Wananchi pindi wanapotumia barabara ikiwemo kuvuka wasivuke
huku wakichat au kuongea na simu, kutakuwa na misafara ya magari hivyo
wawe makini" alisema
Alisema
Jeshi la Polisi limejipanga kudumisha Ulinzi kipindi chote cha
maonyesho hayo huku akitoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto na
nyumba za kulala wageni kudumisha Ulinzi kwenye maeneo yao, kwani mara
nyingi kumekuwa na matukio ya upororaji wa kompyuta na mali.
Maonyesho
ya Utalii Kusini yanatarajiwa kufunguliwa Septemba 20 na Rais wa
Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi Do. Ali Muhamed Shein kwenye viwanja
wa Kihesa Kilolo.
No comments:
Post a Comment