Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, akipiga mpira wa kichwa ambao
uliipatia bao la kwanza timu yake kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania
bara (VPL), dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba
mjini Bukoba jana. Simba ilishinda mabao 3-0. (Picha na Simba SC).
Na Alodia Dominick, Bukoba
Simba imeibuka kidedea baada ya kuichapa Kagera Sugar 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliofanyika katika Uwanja wa Kaitaba.
Mabao mawili ya Simba yamefungwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Meddie Kagere, katika dakika ya 4 na 78 ambapo bao la pili alifunga kwa mkwaju wa penalti.
Bao la pili lilifungwa na beki wa Simba, Mohamed Hussein katika dakika ya 35 na kuzima kabisa ndoto za Kagera Sugar.
Ushindi huo unaifanya Simba kukaa kileleni mwa ligi ikiwa napointi tisa (9), sawa na Kagera Sugar lakini wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga.

No comments:
Post a Comment