HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 18, 2019

TMA yajipanga kutoa elimu SADC

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya hali ya Hewa Tanzania (TMA) imejipanga kupokea wageni kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kutokana na ubora wa huduma zao.

Kaimu Meneja wa Huduma za Utabiri TMA, Wilberforce Kikwasi, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumzia ubora wa huduma na kasi ya wataalam wa hali ya hewa kutoka SADC wanaotembelea banda la mamlaka hiyo baada ya kuelezwa kwamba taarifa za mamlaka zina uhakika kwa asilimia zaidi ya 80.

"TMA katika mkutano huu tunawaonyesha wenzetu namna tunavyofanya kuyafuta kuchakata na kutoa taarifa za hali ya hewa kwa wananchi.., nchi yetu inatumika kimkakati katika ukanda huu na hii ni kutokana na miundombinu tuliyonayo ambayo serikali imetusaidia sana," alisema Kikwasi.

Alisema kwa wananchi hapa nchini wana nafasi kubwa ya fursa za kiuchumi kwa kufuatilia na kuzitumia taarifa za hali ya hewa.

"Biashara pia zinategemea sana taarifa za hali ya hewa.., na shughuri nyingine pia za kimaendeleo, TMA tunawashauri wananchi wafuatilie taarifa tunazozitoa," alisema.
Kwa mujibu wa Kikwasi, TMA pia imepata uzoefu kwenye mkutano huo kwa nchi zinazopata majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Hivi karibuni Msumbiji  walikumbwa na kimbunga Keneth, tunapata uzoefu na kujifunza namna walivyokabiliana nacho."

Alisema maendeleo ya wakati ujao kwa Tanzania, SADC na nchi zote za Afrika zinategemea zaidi taarifa za hali ya hewa hivyo wadau na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuzifuatilia.

No comments:

Post a Comment

Pages