Mkurugenzi wa Shirika la kwa Wazee Nshamba, Bi Lydia Lugazia.
Mgeni rasmi chrizant Kamugisha.
Meneja wa Mradi wa Vijana Bicycle Center, Adelphinus Alexander.
Na Lydia Lugakila
Ili kukomesha vitendo vishawishi vinavyowakumba watoto wa kike wawapo njiani vitokanavyo
na kutembea umbali mrefu kufuata Elimu,
shirika lisilo la kiserikali la kwa wazee Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera
limetoa baiskeli 100 bure zenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa wanafunzi wa kike wapatao 100 kutoka shule za
sekondari 25 wilayani humo ili
kuwawezaesha wanafunzi hao kupata elimu
bila vikwazo.
Zoezi hilo la ugawaji wa baiskeli bure
kwa wanafunzi hao kutoka shule 25 za
sekondari za wilaya hiyo limefanyika Septemba 20, 2019 katika uwanja wa Zimbihile uliopo wilayani Muleba kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi hasa
wale wanaotembea umbali mrefu kwenda shule na kupunguza mimba za utotoni
zinazotokana na vishawishi wavipatavyo njiani.
Adelphinus Alexander ni Meneja wa Mradi wa Vijana Bicycle Centa Center
(VBC) chini ya Shirika la kwa Wazee
Nshamba amesema kuwa wilaya ya muleba imekuwa ikitajwa mara kwa mara kuhusika
na vitendo vya mimba za utotoni jambo ambalo husababisha watoto wa kike
kushindwa kufia ndoto zao huku wengi
wakiishia katika vishawishi vya kupewa lifti na waendesha pikipiki ambao
huaribu maisha yao kabla ya kutimiza ndoto zao.
Kufuatia hali hiyo Alexander na timu
yake kutoka shirika hilo wameamua kupambana vikali ili kutokomeza kabisa
vitendo hivyo kwa kutoa Baiskeli 100 kwa watoto hao wa kike toka shule za
sekondari 25 za wilaya hiyo ambapo pia zimetolewa taa za solar 240, mashine 26 za kuongeza usikivu kwa watooto
wenye ulemavu pamoja bima za afya zipatazo 60 kwa wanafunzi kwa ajili ya kujisomea vitu vinavyokamilisha jumla ya shilingi
milioni 23.
Bi Lydia Lugazia ni Mkurugenzi wa Shirika la kwa Wazee Nshamba amesema
shirika hilo limekuwa ni mdau wa maendeleo wilayani hapo kwa kipindi cha miaka
16 ambapo licha ya kujizatiti katika huduma za kuongeza kinga kwa jamii,
ikiwemo kutetea , kulinda na Kusaidia
wazee na watoto lengo lao ni kuongeza
ustawi kisaikolojia katika kuhakikisha
watoto wote wananufaika katika Nyanja ya
Elimu.
Bi Lugazia amesema kuwa shilika hilo
limekuwa likitoa vifaa vy shule kwa watoto wenye mahitaji maalum ambapo jumla
ya walengwa 107 wakiwa wasichana 56 wavulana 51 wanahudumiwa ndani ya Kata ya 6
ambazo ni Ngenge, Biirabo, Mubunda, Kashasha, Nyakatanga na Mshabago
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika zoezi hilo Chrizant
Kamugisha ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amelishukuru
shirika hilo katika mapamabano hayo yanayolenga kutokomeza mimba za utotoni na
kuyataka mashirika mengine kuiga mfano kama huo na huku akiwahimiza wazazi wa wanafunzi hao kutotumia baiskeli
hizo katika shughuli zao binafsi bali zitumike kwa wanfunzi hao tu kwenda shule ili kutimiza ndoto zao.
Hata hivyo wadau wa elimu na wazazi wa
wanafunzi hao wamewahimiza watoto hao kusoma kwa bidii na kuwa na neno hapana
Mdomoni mwao mara wanapokutana na vishawishi vya aina mbali mbali.
No comments:
Post a Comment