Wachezaji
Kutoka kulia Merci Nyanchama wa Kenya Peace Kabasweka wa pili
kulia wakibadilishana matokeo na Angel Eaton wa kwanza kushoto na
Hawa Wanyenche wa pili kushoto wote wa Lugalo mara baada ya kumaliza
mchezo kwa Siku ya pili ya mashindano ya wazi ya Wanawake Tanzania
katika Uwanja wa TPC Moshi. (Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Wachezaji
Merci Nyanchama wa Kenya na Peace Kabasweka kulia na Angel
Eaton na Hawa Wanyenche kushoto wa Lugalo wakipongezana mara baada
ya kumaliza mchezo kwa Siku ya pili ya mashindano ya wazi ya Wanawake
Tanzania katika Uwanja wa TPC Moshi (Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu
Mashindano ya golf ya wanawake Tanzania yamefikia siku ya
pili huku wachezaji kutoka klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya
Lugalo wakichuana vikali na mchezaji kutoka Uganda Peace Kabasweka.
Mchezaji huyo wa Uganda
aliongoza tangu siku ya kwanza kwa fimbo mbili dhidi ya Angel Eaton wa Lugalo
akifuatiwa na Hawa Wanchenche wa Lugalo pia.
Licha ya kuongoza kwa fimbo mbioli siku ya kwanza
mchezaji huyo kutoka uganda alisema bado mchezo ni mgumu na matumaini ya
kuibuka na ushindi bado ni magumu na mwamuzi ni siku ya mwisho ya mchezo
“ Wachezaji kutoka Lugalo ni Wakali na Wanajituma na Idadi ya Fimbo ninazoongoza ni chache hivyo
ukifanya mzaha kidogo basi ni rahisi kufungwa hivyo bado naweza kusema Mchezo
ni Mgumu” Alisema Kabasweka
Naye Mchezaji kutoka Lugalo Angel Eaton aliyekuwa
akimfuatia alisema peace ni Mchezaji mzuri na mchezo bado uko upande wake
lakini hakuna kukata tamaa mpaka dakika ya mwisho.
“ Nimetumwa na klabu yangu ushindi hivyo nitapambana
kuhakikisha ubingwa unakwenda lugalo
mengine tumwachie mungu kwani kuna wachezaji wazuri tu na wanacheza vizuri
mpaka sasa “ Alisema Angel.
Kwa Upande wake mchezaji Hawa Wanchenche naye kutoka kutoka klabu ya Lugalo alisema wamepangwa kundi moja leo kutokana na mchezao mzuri na hapa tunawania ubingwa
lakini pia nafasi kushiriki mashindano nchini Uganda.
Kutoka Kenya ambao nao wameshiriki katika mashindano haya mchezaji Merci Nyanchama
kutoka kwa upande wake alisema amecheza vibaya hivyo hana matumaini ya ushindi
lakini kiujumla mashindano ni mazuri na yamevutia.
No comments:
Post a Comment