HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 01, 2019

MWAKYEMBE AMPONGEZA MKUU WA MAJESHI KULETA MAPINDUZI KWENYE GOFU

Na Luteni Selemani Semunyu
 
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa kuendeleza Mchezo wa Golf nchini ambao umekuwa ukileta heshima kubwa kwa ushindi Ndani na Nje ya nchi hasa kwa Timu ya Wanawake.

Waziri Mwakyembe alisema hayo Mwisho wa Wiki Akifunga mashindano ya Wazi ya wanawake Tanazania Ladies Open yaliyoshirikisha Wachezaji zaidi ya 50 kutoka Kenya Uganda na Wenyeji Tanzania katika Uwanja wa TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro

Waziri Mwakyembe alisema analishukuru JWTZ anashukuru Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo na Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu kwani amekua akishuhudia mapinduzi makubwa ya Mchezo huo kwa Timu ya Lugalo ikiibuka na Ushindi mkubwa katika mashindano Mengi sambamba na mashindano yanayoshirikisha Timu ya Taifa ya Gofu Lugalo wakiwemo. .

Aliongeza kuwa sasa wanaangalia nini cha kufanya kwa kundi la Wanawake wakiwemo wachezaji wanawake wa Gofu kutokana na mafanikio ya Timu hizo zinzposhiriki katika mashindano ya Kimataifa ukilinganisha na Wanaume.

“ Jeshi linafanya kazi Kubwa na niseme tu Timu za Wanawake ndio timu Pekee zilizotuletea heshima na Vikombe kwa Mwaka huu ikiwemo Timu ya Taifa ya Golf na Timu ya Golf ya Lugalo lakini pia katika Soka ni Wanawake na Katika Mpira wa magongo hivyo lazima kuwapongeza na kuwaunga mkono” alisema Waziri Mwakyembe.

Katika mashindano hayo ya Wanawake Klabu ya Gofu ya JWTZ ya imenyakua Vikombe nane kati ya 15 katika Mashindano wakiongozwa na Angel Eaton aliyeshika nafasi ya Tatu kwa mikwaju gross 235 na Hawa Wanyenche aliyeshika nafasi ya Nne kwa Gross ya 236 baada ya Mchuano Mkali na Peace Kabasweka aliyepata Mikwaju Gross 226 kuibuka na Ushindi akifuatiwa na Irene Nakalembe kwa Mikwaju 232 wote kutoka Uganda

Kwa upande wa kundi la Bronze ambalo kwa kupiga mikwaju washindi ni Private Hadija Selemani aliyefatiwa na Private Amanda Mlula na watatu ni Private Zumla Hamisi huku uande wa Mikwaju ya Jumla kwa kundi la Silver na Bronze Salma Juma wa Lugalo aliibuka na Ushindi wa kwanza akifuatiwa na Happy Castro naye wa Lugalo.

Kwa upande wa watoto Mchezaji wa Lugalo Christina Charles aliibuka mshindi huku nafasi ya Pili ikichukuliwa na Aaraji Somji wa Klabu ya Arusha Gymkhana.

Vikombe vingine ni Washindi wa Kila Siku ambapo Siku ya Kwanza Merci Nyanchama wa Kenya aliibuka na Ushindi wakati siku ya Pili Neema Ulomi wa Arusha alishinda na Siku ya Tatu Nancy Wairimi kutoka Kenya aliongoza.

Kwa Upande wake rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake TLGU Sophia Vigo aliomba wadhamini kuuunga mkono jitihada za wachezaji wa Gofu kwani kwa miaka Zaidi ya Sita hakukuwa na Mashindano kama haya.

Naye Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu aliwataka Wachezaji Wanawake kuendelea kupambana na kuwakilisha nchi vyema kwani mambo mazuri huja baadaya ya kazi nzuri na uwepo wa Waziri mwenye dhamana katika Mashindano yao ni Ishara Wametambuliwa juhudi zao.

No comments:

Post a Comment

Pages