HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 07, 2019

NMB MOBILE, KLIK SASA NI NMB MKONONI


Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni mpya ya dijitali katika kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama NMB Mkononi. Uzinduzi huo umefanuika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. 
 Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, wakizindua kampeni mpya ya dijitali ya kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama NMB Mkononi. Uzinduzi huo umefanuika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, wakizindua kampeni mpya ya dijitali ya kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama NMB Mkononi. Uzinduzi huo umefanuika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kulia), akipeana mkono na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, mara baada ya uzinduzi wa kampeni mpya ya dijitali ya kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama NMB Mkononi. Uzinduzi huo umefanuika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ruth Zaipuna, wakizindua kampeni mpya ya dijitali ya kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama NMB Mkononi. Uzinduzi huo umefanuika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.





NA SALUM MKANDEMBA

BENKI ya NMB imezindua kampeni mpya ya dijitali katika kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama NMB Mkononi, iliyotokana na kuunganishwa kwa huduma mbili za NMB Mobile na NMB KLiK, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kwa watumiaji wa simu za mkononi.

Uzinduzi wa NMB Mkononi, ulifanyika jana Makao Makuu ya NMB, jijini Dar es Salaam, ambako ilielezwa kuwa huduma hiyo inalenga kuwahakikishia Watanzania wote fursa ya kushughulikia masuala ya kibenki kwa urahisi katika viganja vya mikono yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa NMB, Filbert Mponzi, alisema benki yake ilikuwa na huduma za kibenki kwa njia ya simu, lakini imeona umuhimu wa kufanyia kazi mapendekezo ya wateja wao.

“Kwa kuwajali wateja wetu wengi, walioko nchi nzima mijini na vijijini, tukaona ni vema kuchukua mapendekezo yao ya kubadili NMB Mobile na NMB KLiK kuwa NMB Mkononi. Najua wapo watakaojiuliza kwa nini NMB Mkononi?

Mponzi alifafanua hilo na kuongeza maana yake ni Benki Katika Mkono Wako, ambako mteja anapata huduma zote za kibenki katika mkono wake, kupitia simu yake, wakati wowote, mahali popote kwa wepesi, urahisi na usalama. 

“Kwa kuwa kipumbele chetu kikuu ni kuwasaidia Watanzania wote, hata walioko vijijini, kutumia lugha wanayoielewa, tukaona ni vizuri tuje na ‘brand name’ ambayo itawakilishwa kwa Kiswahili na wateja wetu wataona urahisi wa kuijua na kuitumia huduma hiyo,” alisisitiza.

Mponzi alizitaja baadhi ya huduma zinazoweza kupatikana kupitia NMB Mkononi kuwa ni pamoja na kufungua akaunti ya benki hiyo, kutuma na kupokea pesa, kutoa pesa bila kadi ya ATM, kuhamisha pesa kutoka benki moja kwenda nyingine, kulipia bili, tozo na kodi mbalimbali za Serikali.

Aidha, alibainisha kuwa, maboresho hayo ya kihuduma, yataongeza mtazamo chanya wa NMB katika kukuza uwezo na nguvu ya huduma za kifedha zinazotolewa na benki hiyo, ikiwa ni shemu ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja chini ya kaulimbiu yao ya – Ubora Uko Hapa!
NMB Mkononi inatarajiwa kufanya mapinduzi chanya katika kuongeza idadi ya wateja NMB, kutoka Milioni 3.5 wa sasa.

 Benki hiyo pia ina matawi 230 kote nchini, ikiwa na Mawakala zaidi ya 7000 na mashine za kutolea fedha (ATM) 800.

No comments:

Post a Comment

Pages