Na Mwandishi Wetu
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amefanya
ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo Wilaya ya Kinondoni ambapo akiwa
katika Mradi wa Maboresho ya Mto Ng'ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32
ukiwa na urefu wa Km 7.5 amechukizwa kuona hakuna chochote
kinachoendelea kwenye mradi licha ya Viongozi wa Wilaya kumdanganya kuwa
Mkandarasi yupo Site anaendelea na kazi wakati wa kikao kazi
kilichofanyika siku 6 zilizopita kwenye ukumbi wa Karimjee.
Kutokana
na hilo RC Makonda amemuagiza Mshauri wa Mradi kumuita Mkandarasi huyo
Mara moja ofisini kwake ili aeleze nikwanini kazi haifanyiki wakati
tayari mkataba umesainiwa tokea 16/06/2019.
Aidha
RC Makonda amemuagiza mkandarasi huyo kuhakikisha kazi hiyo inakamilika
na kukabidhiwa ndani ya miezi 10 kuanzia sasa tofauti na miezi 18
waliyoomba huku akiwaonya Watendaji wanaoendelea kumpa taarifa za wongo
kuwa Yeye, Katibu tawala wa Mkoa huo na Kamanda Mambosasa wataendelea
kufanya ziara kwenye kila mradi kujionea kama taarifa wanazoletewa
kwenye karatasi zinaendana na kinachofanyika Site.
Akiwa
kwenye Mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa Magomeni linalogharimu kiasi
cha Shilingi bilioni 8.9, RC Makonda amemtaka mkandarasi kufanya kazi
usiku na mchana ili kuhakikisha Soko hilo linakabidhiwa Mwezi Disemba
mwaka huu.
Pamoja na Hayo
RC Makonda ameielekeza Manispaa ya Kinondoni kuhitisha kikao na
Wafanyabiashara wa soko hilo ili wakubaliane namna ya kuweka jografia ya
soko hilo ikiwa ni pamoja na sehemu za maduka,vizimba na eneo la
kushusha mizigo.
Pamoja
na hayo RC Makonda ametembelea mradi wa Ujenzi wa Soko la Tandale
unaogharimu kiasi Cha shilingi Bilioni 8 na kuelekeza Manispaa ya
Kinondoni kuhakikisha mkandarasi anafanya kazi usiku na mchana ili
kuhakikisha anakabidhi kazi ndani ya Miezi sita kuanzia sasa.
TUKUTANE SITE 2019.
No comments:
Post a Comment