HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2019

SERIKALI KUPITIA MKATABA YA UBINAFISHAJI WA KIWANDA CHA NYUZI TABORA BAADA YA KUBAINI HAKIFANYI VIZURI

NA TIGANYA VINCENT
 
SERIKALI itapitia mkataba wa ubinafsishaji wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora (New Tabora Textile Tanzania Limited) baada ya kutoridhishwa utendaji wa uzalishaji ili kuchukua hatua mapema ambazo zitasaidia kufanyakazi kwa kiwango chake endapo itabainikiwa wawekwenda kinyume kwa masharti yaliyomo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Viwanda na Bisahara Innocent Bashungwa wakati wa ukaguzi wa viwanda mbalimbali mkoani Tabora na kukuta kiwanda cha Nyuzi Tabora kikiwa katika uzalishaji mdogo wakati pamba ya wananchi imejaa mitaani.

Alisema kiwanda hicho kingekuwa kinafanyakazi kulingana na uwezo wake kingesaidia sana kupunguza tatizo la ununuzi wa pamba ya wakulima kususua na kingeongeza uzalishaji wa zao hilo na kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa.

Bashungwa alisema kwa kuwa Mmiliki wa Kiwanda hicho ameonekana kuwa na uwezo mdogo na hivyo awe tayari na maamuzi ambayo yatafikiwa baada ya kuangalia mkataba na vigezo alivyopewa wakati ubinafishaji na ikibainika amekiuka Serikali itachukua hatua ili kuongeza tija na utendaji kazi wake.

Alisema wakati wa Mwekezaji huyo na wengine kuendelea kukalia viwanda ambavyo vilitarajiwa kuzalisha kwa ajili ya kukuza uchumi na kutengeza ajira umekwisha na Serikali itachukua hatua.

“Tutangalia Sheria inasemaje na mkataba mlioingia …ili kuangalia njia bora ya kukifanya kiwanda hiki kifanye kazi kwa ajili ya mustakabali mzuri wa wakazi wa Tabora na nchi kwa ujumla...kwa kweli sijaridhishwa na utendaji wa kiwanda hiki” alisema.

Aidha Waziri huyo alivitaja Viwanda vingine ambavyo uzalishaji na utendaji wake sio mzuri ni pamoja na Mwatex na Mutex ambavyo navyo mikataba ya ubinifsishaji wake itachunguzwa kwa ajili ya kuchukua hatua kuvinusuru.

Awali Mbunge wa Tabora Mjini Emmenuel Mwakasaka alisema toka mwaka jana alipotembelea Kiwanda hicho hakuna maendeleo yoyote ambayo yamefanyika na kukifanya kutokuwa na tija kwa vijana na wakazi wa Tabora.

Alisema toka mwaka jana hakuna ajira hata moja iliyoongezeka zaidi ya mfanyakazi mmoja.

No comments:

Post a Comment

Pages