Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, akielekea katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, Wambura anayekabiliwa na kosa la uhujumu uchumi ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabili. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA JANETH JOVIN
ALIYEKUWA
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura
ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ameandika barua kwa
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na
kukiri makosa yanayomkabili mahakamani hapo.
Wambura
ambaye alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, Februari 11,
mwaka huu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka 17
yakiwemo ya kutakatisha zaidi ya Sh. Milioni 100.
Wambura
alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina kuwa,
ameandika barua hiyo kufuatia agizo la msamaha uliotolewa na Rais John
Magufuli hivyo ameuomba upande wa mashtaka wafuatilie barua hiyo ili
apate majibu kwa haraka.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai watafuatilia suala hilo ili wapate majibu mapema.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16,2019 kwa ajili ya kutajwa.
Wambura
anakabiliwa na mashtaka hayo 17, yakiwemo moja la kughushi, shtaka
moja la kutoa na kuwasilisha nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha
haramu.
Katika shtaka la kwanza ambalo ni
la kughushi, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 6, 2004, sehemu
isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Siku
hiyo, Wambura kwa nia ya kutapeli alitengeneza barua ya kughushi ambayo
haina kumbu kumbu namba akionyesha imeandikwa na E Maganga ambaye ni
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Jeck system anadai kurejeshewa malipo ya
mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba aliyokuwa ameikopesha TFF.
Katika
shtaka la kutoa na kuwasilisha nyaraka ya uongo, mshtakiwa alitoa barua
iliyokuwa haina kumbu kumbu namba ya Julai 6, 2004, akijifanya kwamba
ni barua iliyoandikwa na E. Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Jeck
System Ltd, akionyesha kuwa anadai mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba
waliokopeshwa TFF huku akijua kuwa siyo kweli.
Hata
hivyo, kuanzia shtaka la tatu hadi la 15 mshtakiwa anadaiwa kujipatia
kiasi cha zaidi Sh 95 milioni, kwa njia ya udanganyifu akidai kuwa fedha
hizo ni sehemu ya malipo ya jumla ya kiasi cha fedha mbali mbali na
riba kutoka kwa kampuni ya Jeck System Ltd huku akijua kuwa siyo kweli.
Pia
katika mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, Wambura
anadiawa kutenda kosa hilo, Juni 17, 2015 huko katika ofisi za TFF,
ambapo kwa njia ya udanganyifu, mshtakiwa alijipayia Sh 10milioni kutoka
TFF kwa kuonesha kuwa ni malipo ya USD 30,000 pamoja na riba kutoka
kwenye kampuni hiyo ha Jeck jambo ambalo siyo kweli.
Katika
shtaka la utakatishaji fedha, Wambura anadai, kati ya Agosti 15 na
Oktoba 21, 2014, makao makuu ya Shirikisho hilo, alijipatia Sh 25milioni
kutoka TFF huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.
Pia,
shtaka jingine utakatishaji fedha haramu, Mshtakiwa anadaiwa kati ya
Machi 16 na Oktoba 21 2015, alijipatia Sh 75,947,924 kutoka TFF wakati
akijua fedha hizo siyo halali na zimetokana na shtaka la kughushi.
No comments:
Post a Comment