Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Divas Empowement wakiwa kwenye hafla ya kutimiza miaka mitano ya kikundi hicho.
Mwenyekiti wa Divas Empowement, Marylinda Bawaziri akiwa na kiongozi wa Mfuko wa Shida na Raha, Antonotte Nassoro.
Na Irene Mark, Dar es Salaam
WANAWAKE hapa nchini wameshauriwa kujiunga na kuwekeza kwenye vikundi huku wakifanyabiashara mbalimbali zitakazowaunganisha na kuwainua kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa Oktoba 19,2019 na Mwenyekiti wa kikundi cha Divas Empowement chenye maskani yake jijini Dar es Salaam, Marylinda Bawaziri wakati wa hafla ya kutimiza miaka mitano ya kikundi hicho.
Alisema wanawake ni jeshi kubwa linaloweza kufanya mambo makubwa kiuchumi katika taifa hivyo waache kujishusha na kusubiri kupewa fursa hata wanazoziona wazi.
"Kuna usemi kwamba mtu tajiri ni mfanyabiashara sio mwajiriwa hii kauli naielewa sana, ukisema umeajiriwa ukabweteka kusubiri mshahara utakufa maskini.
"...Sisemi kuajiriwa ni kubaya, hapana ila unapokuwa huko jicho lako liione ajira yako kuwa fursa ya kufanyabiashara yoyote utakaifanya bila kuingilia muda wa kazi zako," alisema Bawaziri.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, biashara nyingi za wanawake zinakufa kwa majungu na kutopenda wao kwa wao hivyo kushindwa kuungana mkono.
Alitumia fursa hiyo pia kuwashauri wanadivas kuongeza nguvu kwenye mfuko wao wa shida na raha aliodai kuwa kimbilio la faraja kwa wanakikundi wote wanapofikwa na jambo.
"Huu ni mfuko wetu wote unatuunganisha kwenye jambo zuri au changamoto inayomkuta mmoja wetu hivyo tusiache kuchangia na tuuthamini," alisema mwenyekiti huyo aliyejinadi kuwa mjasiriamali wa bidhaa mbalimbali.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo kiongozi wa mfuko wa shida na raha, Antonette Nassoro, aliwataka wanakikundi hao kumpa ushirikiano na kujitoa zaidi unapotokea wakati wa kumtembelea mwanakikundi aliye kwenye changamoto.
Wanakikundi hao ni wanawake kutoka ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam wanaounganishwa na biashara mbalimbali wanazofanya.

No comments:
Post a Comment