Na Mwandishi
Wetu, Kibaha
Benki ya CRDB imetaja
sababu ya kuwa wadhamini wakuu katika Maonesho ya Pili ya Viwanda na Uwekezaji
yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph
Witts, alisema kuwa sababu ya kuwa wadhamini wakuu wa maonesho ya viwanda na
uwekezeaji mkoani Pwani ni mahusiano bora waliyonayo na Serikali kiutendaji.
.
Amesema
hayo leo ikiwa ni siku ya tatu ya maonesho hayo yanayoendelea Kibaha mkoani
Pwani ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa,
alitembelea maonesho hayo na kuzungumza na wadau mbalimbali wa uwekezaji wa
mkoa huo.
Witts
amesema lengo lao ni kuendeleza ushirikiano na Serikali katika kufikia Tanzania
ya Uchumi wa kati ifikapo 2025 yenye mapinduzi makubwa ya Viwanda.
“Tumekuwa
wadhamini kwa mwaka wa pili mfululizo kwani ni dhamira yetu ya kuendeleza
ushirikiano na Serikali katika kufikia uchumi wa viwanda ambavyo vitatufikisha
kwenye Tanzania ya uchumi wa kati ifikapo 2025”.alisema Witts.
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (kushoto), akiwa na Meneja wa benki hiyo tawi la Kibaha, Rose Kazimoto (wa pili kushoto) wakiwasili katika maonesho ya Viwanda na uwekezaji Kibaha mkoani Pwani.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, mara
baada ya kufika katika banda la benki hiyo katika Maonesho ya Pili ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji yanayoendelea katika viwanja vya mkuu wa
Mkoa Kibaha.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika banda la Benki ya CRDB mara baada ya kufika katika banda la benki hiyo katika Maonesho ya Pili ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji yanayoendelea katika viwanja vya mkuu wa Mkoa Kibaha.
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, akitoa maelezo kuhusu benki hiyo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Pili ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji yanayoendelea katika viwanja vya mkuu wa Mkoa
Kibaha.
Ofisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, akizunguma na
wadau mbalimbali wakiwemo wawekezaji walioweke Kibaha mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, akisaimiana na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, alipotembelea banda la Benki ya CRDB.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji.
Picha ya pamoja.
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, akizungumza na wajasiriamali waliodhaminiwa na benki hiyo katika Maonesho ya Pili ya Viwanda na Biashara Kibaha mkoani Pwani. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kibaha, Rose Kazimoto.
No comments:
Post a Comment