HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 29, 2019

BILIONI 19.4 KUTUMIKA UJENZI WA CHUO CHA VETA-KAGERA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prfof. Joyce Ndalichako, akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Bukoba katika eneo kitakapojengwa chuo.
Balozi wa China nchini Tanzania, WANG Ke, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi  Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera. 



Na Alodia Dominick, Bukoba

Zaidi ya shilingi bilioni 19.4 za Kitanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa chuo  cha mafunzo ya ufundi stadi VETA katika kijiji cha Burugo kata ya Nyakato Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera.

Kiasi hicho kimetajwa novemba 28 mwaka huu na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Pankarasi Bujuro wakati akiwasilisha taarifa ya mradi huo kwa mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, katika eneo kitakapojengwa chuo hicho.

Akisoma taarifa hiyo Bujuro amesema mradi unaotekelezwa na kampuni ya Shansi constraction investiment group na kusimamiwa na makampuni ya kichina utaghalimu sh bilion 19.04 ambazo nisawa na dollar millioni 8 za kimarekani na unafadhiriwa na serikali ya China kwa kushirikiana na nchi ya Tanzania.

Akizungumza katika afla hiyo waziri wa Elimu, sayansi na Teknorojia Joyce Ndalichako amesema kuwa, chuo hicho kinajengwa nchini kutokana na msaada wa nchi ya China lakini ni kutokana na uhusiano mzuri baina ya nchi zote mbili China pamoja na Tanzania.

Ndalichako ameeleza kuwa jumla ya watanzania 400 wanatarajiwa kupata ajira katika kipindi cha ujenzi wa chuo hicho pamoja na kupata ujuzi katika kipindi hicho.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia General Marco Gaguti, amewashukuru wananchi  wa kijiji cha Burugo kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika mradi huo na aliwaomba wananchi wa kata ya Nyakato kuhakikisha ulinzi wa eneo la mradi pamoja na vifaa ili kukamilika kwa mradi huo na kwa wakati.

Chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kudahiri wanafunzi 800 wa kozi ndefu za miaka miwili hadi mitatu na wanachuo 2,000 wa kozi fupi zinazo chukua miezi mitatu mpaka 6 pia kinatarajiwa kujenga mabweni mawili,madarasa 14, ofisi za walimu zenye vyumba 9 majengo matatu ya karakana, kumbi mbili za mikutano, jengo la utawala ,jiko na bwalo la chakula, nyumba za walimu na miundo mbinu mbalimbali. 

Eneo lililotolewa na kijiji cha Burugo  ni zaidi ya hekari 100  na mpaka sasa mradi upo katika hatua za awali baada ya kusafisha eneo ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi na nane.

Afra hiyo imeudhuliwa na wananchi, viongozi mbalimbali wa mkoa, wilaya ,kata na  kijiji pamoja  na balozi wa China hapa nchini WANG Ke.

No comments:

Post a Comment

Pages