HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 18, 2019

KILIMANAJARO QUEENS YAICHAPA BURUNDI 4-0

  Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara ‘Kilimajaro Queens’, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ akiwania mpira na beki wa timu ya taifa ya Burundi katika mchezo wa michuano ya Chalenji kwa wanawake uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jana. Kilimanjaro Queens ilishinda 4-0. (Picha na TFF).
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara ‘Kilimajaro Queens’, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ akimchambua mlinda mlango wa timu ya taifa ya Burundi katika mchezo wa michuano ya Chalenji kwa wanawake uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jana. Kilimanjaro Queens ilishinda 4-0. (Picha na TFF).
 
Na John Marwa 

TIMU ya Taifa ya Wanawake Kilimanjaro Queens imezidi kuchanja mbuga katika michuano ya CECAFA Women Senior Championship 2019 kwa kuwachakaza Burundi kwa mabao 4-0.

Unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Kilimanjaro Queens katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Afrika Mashariki na kati kwa Wanawake inayoendelea katika Viwanja vya Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Kilimanjaro Queens yamewekwa kambani na Donesia Minja akiweka kambani mabao mawili dakika za 34 na 65, Asha Rashid Mwalala dakika ya 72 na ,  Mwanahamis Omari 'Gaucho' dakika ya 86.

Kwa ushindi huo Kilimanjaro Queens wamefikisha pointi 6 mechi mbili na mabao 13 wakiwa hawajaruhusu bao. 

Safari ya mwisho katika hatua ya makundi kwa Kilimanjaro Queens wataumana na ndugu zao Zanzibar Novemba 20, ambao wako dhofulihali wakiwa wameaga mashindano hayo kwa kupoteza mechi mbili mtawalia kwa jumla ya mabao 10.

Zanzibar walikubali kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Burundi mchezo wa ufunguzi kisha leo kulala kwa kipigo kama hicho dhidi ya Sudan Kusini.

No comments:

Post a Comment

Pages