HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2019

MAGUFULI; VIONGOZI WASTAAFU CHACHU YA VIJANA KATIKA UONGOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,  Benjamin William Mkapa baada ya  uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Mkapa. Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Dk. Jakaya Kikwete katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Jumanne Novemba 12, 2019. (Picha na Ikulu).
 

Na Asha Mwakyonde

VIONGOZI wastaafu nchini wametakiwa kuwa chachu kwa vijana wanaotamani kuingia katika masuala ya uongozi kwa  kuandika  historia ya maisha yao.

Pia amewahimiza Watanzania kujenga utamaduni wa kujisome vitabu  na kwamba vitakuwa na manufaa yoyote kama havitasomwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo  Novemba 12, 2019 Rais  John Magufuli  wakati wa  uzinduzi wa kitabu cha historia ya maisha ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kilichopewa jina la ‘My life my purpose’ amesema uandishi huo wa vitabu usiishie kwa viongozi wastaafu bali na viongozi wengine wafuate nyao za Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa kuwa ni masuala muhimu katika historia na maendeleo kiujumla.

“Ni vema viongozi wengine wastaafu mkaiga
mfano wa mzee Mkapa kwa kuandika vitabu ili
uzoefu wenu katika uongozi uwe chachu kwa vijana wetu wanaoinukia kwenye uongozi,", amesema Rais  Magufuli.

Amesema kuwa amefurahi  kusikia kuwa mchakato wa kukamilisha kitabu cha Mzee Mwinyi uko mbioni kukamilika
na Mzee Kikwete pia anaendelea na uandishi wa
kitabu chake.

Uzinduzi huo  umehudhuriwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

No comments:

Post a Comment

Pages