Na Ahmed
Mahmoud, Arusha
SERIKALI
imesema kuwa kipindi cha miaka 10 ijayo kuanzia mwakani itahakikisha eneo lote
nchini linapimwa na kutengenezewa misingi ya matumizi bora ya Ardhi kwa lengo
la kuondoa migogoro na kuongeza thamani ya Ardhi sanjari na kutoa hati miliki.
Aidha zoezi
hilo la kupanga matumizi sahihi ya Ardhi linaenda sambamba na kuowanisha sera
za watumiaji wa rasilimali mbalimbali
kama vile misitu maji madini ambazo zote zipo kwenye Ardhi hivyo kuona umuhimu
wa kupanga kwa ujumla matumizi sahihi ya Ardhi.
Akizungumza
kwenye mkutano wa majadiliano ya mandhari ya mazingira na matumizi sahihi ya
Ardhi kwa nchi za Afrika unaoshirikisha nchi zaidi ya 20 za bara la Afrika Waziri
wa Ardhi nyumba na makazi William Lukuvi alisema kuwa mkutano huo ni muhimu na
umekuja wakati muafaka serikali ikiwa kwenye mchakato wa kuandaa upimaji wa
Ardhi nchini.
“Tumeshafanikiwa
kwenye wilaya tatu nza mkoa wa Morogoro ambazo ni Malinyi Ulanga na Kilombero
kupanga kila kipende cha Ardhi na kuwezesha kutoa hati zaidi ya laki tano za
kimila kwa kipndi ncha miaka minne sasa tuaenda kwenye ajenda kubwa ya kupanga
kupima na kumilikisha ardhi ya Tanzania” Alisema Lukuvi
Kwa Upande
wake Mkurugenzi wa Tume ya Taifa mipango ya matumizi bora Ardhi chini ya wizara
ya Ardhi Dkt.Steven Nindi alisema kuwa eneo la Tanzania lina ukubwa wa
takribani kilomita za mraba zipatazo milioni moja hivyo katika mkutano huu
wanaangazia namna ya kupata rasilimali fedha na rasilimali watu ili kuharakisha
zoezi zima la upangaji,usimamizi na utekelezaji wa matumizi bora ya Ardhi.
Alisema
lengo ni kuhakikisha Ardhi nzima hapa nchini inapimwa na kupangwa matumizi bora
na endelevu kwa maendeleo endelevu ya rasilimali za misitu maji madini
kuhakikisha tunakuwa na sera moja itakayosaidia kuondoa wigo na kuhimiza fursa kwa
matumizi bora ya rasilimali mbali za ardhi.
Nae
Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Mipango ya Matumizi bora ya Ardhi
,Wakili Fidelis Mutakyamilwa alisema katika muda wa miaka kumi Taznania
itakuwa imekamilisha mpango wa matumizi bora ya Ardhi ambayo itasaidia
kuondoa
migogoro ya muda mrefu hapa nchini.
Amesema kuwa
mkoa wa Morogoro na Arusha inaongoza kwa migogoro ya ardhi hususani Rasilimali
mifugo kwa mkoa wa Arusha iliyopeleka migorogoro ya wafugaji na wakulima
wakigombea malisho huku wengine wakiwa ndani ya hifadhi hivyo kuleta changamoto
baina ya Tanapa NCAA na wafugaji.
No comments:
Post a Comment