Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa hotuba kwa wadau wa kongomano
la ukatili dhidi ya watoto mkoani Tanga.
Na Mwandishi Wetu, Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Bw. Martine Shigela amekemea tabia ya Wazazi, Walezi pamoja na Jamii ya Mkoa wa
Tanga kukumbatia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto jambo ambalo linasababisha
mkoa huo kuwa na takwimu za juu za vitendo vya ukatili kuliko mikoa mingine.
Mkoa wa Tanga kwa
mujibu wa takwimu za jeshi la Polisi hapa Nchini unaongoza kwa vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto ndio maana Wizara ya Afya pamoja na wadau wameamua
kuweka kongamano la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani humo ili
kujadiliana namna bora ya mkoa huo kuondokana na changamoto hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga
katika hotuba yake kwa wadau wa kongomano hilo amesema ni vitendo vya haibu kwa
wakazi wa mkoa huo kuendelea kutajwa kuhusiana na ukatili dhidi ya watoto na
hivyo kuwataka wadau wa kongamano hilo kuja na mkakati utakaowezesha mkoa huo
kuweka mikakati ya kupambana na hatimaye kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya
watoto mkoani humo.
Aidha Mkurugenzi wa
Watoto Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza amesema
kimsingi Kongamano hilo linafanyika Mkoani Tanga kutokana na Mkoa huo kuongoza
kwa vitendo vya ukatili hapa Nchini akiongeza kuwa kongamano hilo linahusisha watoto,
viongozi wadini na wazee mashuhuri wa mkoa huo ili kwa pamoja kutafuta namna
bora ya kutokomeza vitendo hivyo.
Aidha Bi. Magwiza
ameviambia vyombo vya habari kuwa Kongamano hilo lianaangazia changamoto ya
ukatili dhidi ya watoto kama janga kubwa ambalo kimsingi halinabudi kuangaliwa
upya kwa mustakabali wa ustawi wa maisha ya baadae ya mtoto.
Bi. Magwiza ameyataja
maeneo manne ambayo Wizara yake na wadau watatotoa kwa ajili kuelimisha
Kongamano hilo kuwa ni eneo la ukatili kwa ujumla wake, wajibu wazazi na walezi
katika makuzi ya mtoto,ukatili wa watoto mtandaoni pamoja na umuhimu wa malezi
na makuzi kwa ajili ya maendeleo ya mtoto.
Wakati huo huo
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wiazara ya Afya Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akifafanua
zaidi kuhusu ukatili wa watoto mitandaoni ameonya wazazi na walezi hapa Nchini
kuwa makini na watoto wakati wa matumizi ya vifaa vya kielektroniki kwani vifaa
hivyo vinatumika katika kuendeleza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Bw. Kitiku ameliambia
kongamano hilo kuwa watoto ni weledi sana katika matumizi ya simu pamoja na
television za kisasa na wanatumia muda mwingi katika vifaa hivyo akizitaja simu
kuwa tishio kwani watoto wanapata ukatili wa kingono mtandaoni kupitia
mawasiliano ya simu na kompyuta na kupelekea wengine kujiua baada ya kukosa
usaidizi baada kufanyiwa ukatili na watu wasio wajua.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto kila ifikapo leo tarehe 20 Novemba uungana na nchi nyingine Duniani
kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Haki za Mtoto pamoja na kusherehekea miaka 30
ya utekekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto ndiyo dhana ya
kongamano hili ambalo limefanyaika leo ili kutoa fursa kwa wadau wengi zaidi
kushiriki kuadhimisha siku hii.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto
ulipitishwa rasmi na nchi wanachama wa umoja huo mnamo tarehe 20 Novemba, 1989
sambamba na uanzishwaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (Child Rights Convention) ambapo hadi
sasa nchi 190 wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo zimetia saini na kuridhia
mkataba huu.
No comments:
Post a Comment