HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 14, 2019

MOI yafanya upasuaji wa kwanza kwa mtoto mwenye kifafa

Madaktari bingwa wa MOI kwa kushirikiana na Madaktari bingwa kutoka hospitali ya Chuo kikuu cha Weill Cornell Marekani wakifanya upasuaji wa Ubongo kwa mtoto mwenye ugonjwa wa kifafa leo.


Na Asha Mwakyonde

TAASISI ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI),kwa mara imefanya upasuaji mkubwa wa Ubongo kwa mtoto mwenye  kifafa.

Upasuaji huo umefanywa na madaktari bingwa MOI   kwa
ushirikiana na Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Chuo kikuu cha Weill Cornell cha nchini Marekani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 14,2019 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi  hiyo  Dk. Respicious Boniface amesema hiyo ni hatua kubwa katika matibabu ya Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu hapa nchini kwani awali wagonjwa wenye ugonjwa wa kifafa wanaohitaji upasuaji walikua wanapelekwa nje ya nchi hivyo kuigharimu Serikali fedha nyingi.

Amesema juwa  leo ni siku ya nne ya kongamano  la kimataifa la madaktari bingwa wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya fahamu.

"Kila mwaka wenzetu hawa kutoka mataifa  Marekani na Ulaya wamekua wakituletea teknolojia mpya na hii ya upasuaji kwa wagonjwa wenye kifafa ni mojawapo,"  amesema Dk.Boniface.

Kwa upande wake daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo MOI Dk. Japhet Ngerageza amesema upasuaji huo umewezekana kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa ambavyo vinunuliwa na Serikali ya awamu ya tano.

"Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh Dk. John Pombe Magufuli kwa uwekezaji mkubwa iliyofanya katika taasisi yetu ya MOI, tunaweza kufanya upasuaji kama huu kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi kama EEG, MRI na darubini ya kisasa ya upasuaji wa ubongo ambavyo vyote vimenunuliwa na Serikali, " amesema  Dk. Ngerageza.

Naye  daktari bingwa wa Ubongo aliyeobobea kutibu magonjwa ya kifafa kutoka nchini Kanada Dk.Evan Lewis amesema ni heshma kubwa kuwa sehemu ya kongamano ambalo limepelekea kuanzishwa kwa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wa kifafa hapa Tanzania jambo ambalo litaokoa maisha ya watoto wengi

Ameongeza kwambs upasuaji huo utachukua masaa matatu hadi manne.

No comments:

Post a Comment

Pages