HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 14, 2019

Serikali Yaboresha Utoaji Huduma za Vivuko Nchini

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wakala huo kwa kipindi cha miaka minne toka Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa Taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma

Serikali imepiga hatua katika utoaji huduma za vivuko kwa asilimia 131 huku huduma za karakana zikizidi kuimarika nchini tangu Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) uanzishwe mwaka 2005.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma.
“Wakala umeendelea kuboresha na kusimamia uendeshaji wa vivuko vya Serikali nchini kwa kuongeza idadi ya vivuko kutoka 13 wakati Wakala unaanzisha mwaka 2005 hadi kufikia 30 katika vituo 19 Tanzania Bara,” alisema Mhandisi Maselle. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli. Kutoka kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari – MAELEZO, Jonas Kamaleki na kushoto ni Afisa Habari wa TEMESA, Bi. Theresia Mwami.[/caption] [caption id="attachment_48843" align="aligncenter" width="750"] Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle akionyesha ramani ya maeneo ambapo TEMESA inaendesha vivuko wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.


Akizungumzia mafanikio iliyopata ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mhandisi Maselle amesema kuwa Wakala umefanikiwa kununua vivuko vipya vitatu ambavyo ni MV KAZI kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni mkoani Dar es Salaam,kilichogharimu sh bilioni 7.3, MV MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza kilichogharimu shilingi bilioni 8.9 na MV TANGA kinachotoa huduma kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga ambacho kimegharimu shilingi bilioni 4.02.

Ujenzi wa Vivuko vyote umegharimu jumla ya shilingi bilioni 20.22 ambazo ni fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Ameongeza kuwa pamoja na utoaji wa huduma za vivuko Serikali imenunua boti ndogo tano ambazo ni MV TANGAZO inayotoa huduma ya dharura kati ya Kilambo na Namoto mkoani Mtwara, MV KUCHELE kinachotoa huduma ya dharua kati ya Msangamkuu na Msemo mkoani Mtwara, MV MKONGO kinachotoa huduma kati ya Utete na Mkongo mkoani Pwani, MV BWENI inayotoa huduma dharura kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga pamoja na MV SAR III ambapo ujenzi wa boti zote umegharimu shilingi milioni 415.
Aidha amesema kuwa pamoja na uwepo wa vivuko hivyo TEMESA inaendelea na ujenzi wa vivuko vipya kwa ajili ya maeneo ya Mafia – Nyamisati uaogharimu shilingi bilioni 5.3, Bugorola – Ukara ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni4.2, Chato – Nkome shilingi bilioni 3.1 na Kayenze – Bezi shilingi bilioni 2.7
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi, Japhet Maselle (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli. (Picha zote na: Idara ya Habari - MAELEZO).

Akizungumzia huduma za karakana, Mhandisi Maselle amesema kuwa hadi sasa TEMESA ina karakana 26 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na moja iliyopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambayo imejengwa mahususi kusogeza huduma kwa wateja wa Wilaya za Mlimba, Malinyi na Ifakara ambazo ziko mbali na karakana ya mkoa wa Morogoro.

Amesema kuwa katika kuboresha huduma za karakana Wakala umeanzisha karakana inayotembea ambayo imegharimu shilingi milioni 95 na ambayo itakuwa ikitoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Karakakana hii inayotembea pia itahudimia kwa makundi magari ya Bohari ya Dawa (MSD) yapatayo 100, pia itatoa huduma mkoani Pwani katia wilaya za Bagamoyo, Utete, Mkuranga, Kisarawe pamoja na kutoa huduma ya dharura kwa magari ya umma maeneo ya barabara ya Morogoro.

Wakala umefanikiwa kununua vitendea kazi vya karakana vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni 260 ambavyo tayari vimeanza kusambazwa katika karakana 12 zilizopo Katavi, Geita, Songwe, Pwani, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Rukwa, Morogoro, Kahama, Ifakara, Singida na Lindi.

Katika hatua nyingine Mhandisi Maselle amemshukuru Rais Dkt. Jon Pombe Magufuli kwa kutoa fedha zote bilioni 15 zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa vivuko na kusema kuwa hiyo ndiyo dhamira halisi ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

No comments:

Post a Comment

Pages