Mkuu wa
Wilaya ya Gairo, Siriel Mchemba (Mwenye miwani) akipokea moja ya vifaa
tiba kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki - Baraka Ladislaus kwa
ajili ya kituo cha afya Gairo mkoani Morogoro.
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya na Mganga
M.fawidhi wa kituo cha afya Gairo, Dk. Dastan Mshana.
Meneja wa NMB Kanda ya Kusini - Janeth Shango akikabidhi msaada wa bati 175 kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea-
Pololet Mgema kwa niaba ya shule ya Msingi Ndelenyuma katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi - Sospeter Magese, Akikabidhi msaada wa Bati za Shule za Sekondari na Msingi
kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Erick Komanya. Benki ya NMB ilikabidhi
viti na meza kwa shule za sekondari, vifaa vya unjenzi - bati 216, mbao
na misumari kwaajili ya shule za msingi Kanyenye, Kalunde na Ikomwa
vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 30.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi - Sospeter Magese, Akikabidhi msaada wa Bati za Shule za Sekondari na Msingi
kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Erick Komanya. Benki ya NMB ilikabidhi
viti na meza kwa shule za sekondari, vifaa vya unjenzi - bati 216, mbao
na misumari kwaajili ya shule za msingi Kanyenye, Kalunde na Ikomwa
vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 30.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe - Cornel Magembe akipokea vitanda na mashuka kutoka kwa Meneja wa NMB
Kanda
ya Ziwa - Abraham Augustino (aliyevaa suti), wakati wa hafla ya
makabidhiano yaliyofanyika juzi wilayani Ukerewe. Benki hiyo imekabidhi
msaada wa vitanda na mashuka kwa Hospitali ya Wilaya
ya Ukerewe, viti na meza za shule na chuo cha Murutunguru,vifaa vya
ujenzi kwa Zahanati ya Bwasa na shule za msingi na Sekondari za wilaya
ya Ukerewe vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 75.
NA MWANDISHI WETU
KATIKA kuunga juhudi za utatuzi wa changamoto zinazoikabili
Sekta ya Afya na Elimu nchini, Benki ya NMB wiki iliyopita ilikabidhi misaada
mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Milioni 110 katika wilaya za Songea,
Tabora na Ukerewe.
Thamani ya misaada hiyo ya vifaa vya ujenzi na vifaa tiba,
vinaifanya Benki ya NMB kutumia zaidi ya Sh. Mil. 900 kununulia na kukabidhi
vifaa hivyo kwa Shule za Msingi, Sekondari, Zahanati na Vituo vya Afya nchini
kwa mwaka huu. - 2019
Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, NMB imekabidhi misaada ya vifaa
vya ujenzi, elimu na afya yenye thamani ya Sh. Mil. 75 kwa shule 14 za msingi
na sekondari, Chuo cha Ualimu Marutunguru na Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.
Msaada huo, ulitolewa na Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Augustino
Abraham na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo (DC), Corneli Magembe, ambaye
aliishukuru benki hiyo kwa uwezeshaji huo, alioutaja kama unaoenda kumaliza
tatizo la uhaba wa vifaa kwa taasisi husika.
Mkoani Tabora, NMB imekabidhi viti na meza wenye thamani ya Sh.
Mil. 30 kwa shule sita za Manispaa ya Tabora, tatu zikiwa ni za sekondari na
nyingine tatu za msingi, msaada ambao ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora,
Erick Komanya.
Hafla hiyo ilifanyika Sekondari ya Wavulana Tabora, ambako
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magese, alikabidhi mabati 216, mbao
na misumari vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 15, kwa ajili ya Shule za
Msingi Kanyenye, Kalunde na Ikomwa.
Aidha, NMB ikatoa msaada wa mabati 175 ya geji 28, yenye thamani
ya Sh. Mil. 5, kwa ajili ya Shule ya Msingi Ndelenyuma, iliyopo katika
Halmashauri ya Madaba, wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza kabla ya kukabidhi bati hizo katika hafla ambayo
ilifanyika katika Shule ya Msingi Ndelenyuma, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini,
Janeth Shango, alisema kwa miaka kadhaa sasa NMB imekuwa mstari wa mbele
kuchangia miradi ya mbalimbali ya maendeleo.
“Mpaka ninavyoongea leo, kwa mwaka huu 2019 pekee, tayari NMB
tumetoa misaada yenye thamani ya Shilingi Milioni 900, tumejikita zaidi kwenye
miradi ya elimu, afya na majanga,” alisema Shango wakati wa hafla ya
makabidhiano hayo yaliyofanyika wilayani Songea.
No comments:
Post a Comment