HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 05, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA MABOLOZI WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC WALIOPO NCHINI, WAANDISHI WA HABARI

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)  akiwaelezea waandishi wa habari maandalizi ya mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 - 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya mabalozi kutoka nchi za Afrika na Nordic wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani) wakati alipokutana nao kuzungumzia maandalizi ya mkutano wa 18 wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)  akizungumza alipokutana na waandishi wa habari kuwaelezea Maandalizi ya mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 - 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kikao cha pamoja na mabalozi kutoka nchi za Afrika na Nordic wakizungumzia maandalizi ya mkutano wa 18 wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika tarehe 7 - 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages