Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza wafugaji wote wanaomiliki
maeneo yenye hati kuweka uzio katika maeneo yao ili kuepuka mifugo yao
kwenda maeneo ya wakulima na kusisitiza kufanyika ufugaji wa kisasa.
Lukuvi
alitoa agizo hilo wilayani Kilosa mkoani Morogoro wakati akizungumza na
uongozi wa wilaya ya Kilosa na watendaji wa sekta ya ardhi katika
wilaya hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara ya kutatua migogoro ya
ardhi katika mkoa wa Morogoro.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na
uongozi wa wilaya ya Kilosa pamoja na Watendaji wa sekta ya ardhi katika
wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wakati wa muendelezo wa ziara yake ya
kutatua migogoro ya ardhi mkoani Morogoro.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ameomba kufanyika
ukaguzi wa ardhi za vijiji kwa kuwa baadhi yake watu wamejimilikisha,
wameuza na mengine kufanyika mgawanyo usio sahihi.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William
Lukuvi amesema vijijji viwili vilivyosajiliwa katika maeneo ya hifadhi
wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro vitaendelea kubaki katika maeneo hayo
kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia vijiji 920
vilivyokuwa katika maeneo ya hifadhi kuendelea kubaki maeneo hayo.
Lukuvi
amevitaja vijiji vya Mjambaa kilichoko katika shamba la Mbugani Estates
lenye ukubwa wa ekari 1600 na kile cha Mambegwa kuwa vitaendelea
kutambuliwa na kuagiza halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwenda kuvipima
na kuanisha shughuli za kilimo na makazi katika vijiji hivyo.
No comments:
Post a Comment