Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kwamba Halmashauri Kuu
ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Mwanza chini ya Ndg. John Pombe Joseph
Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkutano huo wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kabla
ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara ya kukagua miradi
mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza. Wajumbe pia walipata
muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka
Minne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Maandalizi na maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 sambamba
na Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania (JMT) inayo ongozwa na Ndugu Rais John Pombe Joseph Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Ndugu
Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM
ambapo mafanikio makubwa ya kimaendeleo yamepatikana.
Halmashauri Kuu ya
Taifa (HKT) imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya
Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama
walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili
yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.
Wanachama hao ni;-
1.
Ndg.
Januari Makamba (Mb)
2.
Ndg.
Nape Nnauye (Mb) na,
3.
Ndg.
William Ngeleja (Mb)
Kikao cha HKT
kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua
kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama
ikiwamo kufukuzwa uanachama.
Wakati uo huo, Halmashauri
Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama
wafuatao;-
1.
Abdulrahman
Kinana
2.
Mzee
Yusuf Makamba na,
3.
Benard
Membe
Waitwe na Kamati ya
Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa
mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.
Awali Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa
nafasi za Uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-
1.
Wagombea
wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha
a.
Ndg.
Batilda Salha Buriani
b.
Ndg.
Zelothe Stephen Zelothe
c.
Ndg.
Bakari Rahibu Msangi
2.
Wagombea
wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa
a.
Mafanikio
Paulo Kinemelo
b.
Hilary
Adelitius Kipingi
c.
Lucas
Felix Lwimbo
3.
Wagombea
wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Mtwara
a.
Petro
Mwendo Mwendo
b.
Mustafa
Nguyahamba Mohamed
c.
Selemani
Manufred Sankwa
4.
Wagombea
wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dodoma
a.
Ndg.
Damas Mukassa Kasheegu
b.
Baraka
Andrea Mkunda
c.
Christopher
Thomas Mullemwah
5.
Wagombea
wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani
a.
Mary
Daniel Joseph
b.
Fredrick
Gasper Makachila
c.
Samaha
Seif Said
Licha ya hamasa kubwa
waliyokuwa nayo wajumbe wa HKT kutokana na kazi nzuri ya Serikali ya CCM, Ndg.
Magufuli amesisitiza kazi ya Urais ni ngumu sana na yeye ataheshimu utamaduni
na desturi za CCM, Kanuni, Katiba ya CCM na Katiba ya Nchi na kwamba CCM ni
kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata
mtu bora zaidi atakayepokea uongozi baada yake.
Nawashukuru sana
viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya Chama chetu kwa kuzisimamia
vizuri Serikali zetu mbili na hivyo kuwezesha kupatikana mafanikio makubwa
katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM. Tukaendelee kujenga umoja, kuimarisha
ujenzi wa Chama chetu na tunapoelekea katika chaguzi zinazokuja tukaepuke
makundi, na tuendelee kuisimamia Serikali ikiwamo kukagua miradi ya kimaendeleo
katika maeneo yetu, amesema Ndg. Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na,
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment