Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo, akipewa maelezo na mjasiriamali
anayezalisha viatu vya ngozi. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk.
Patricia Henjewele.
Mjasiriamali
akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo wakati
akikagua mabanda ya maonesho ya bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchini.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel
Chongolo amesema kuwa katika kutatua changamoto ya kupata soko la uhakika la
bidhaa za ngozi, Wilaya hiyo imejipanga kuwatafutia maeneo wazalishaji wa ndani
ambapo wote watakaa sehemu moja kwa
ajili ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa hizo.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za ngozi yanayofanyika katika viwanja vya
Tanganyika Packers , Mhe. Chongolo amesema kuwa mkakati huo utasaidia kuinua uhakika
wa soko kwa wazalishaji.
Amefafanua kuwa
maonesho hayo ya bidhaa za ngozi yanafanyika kwa mara ya kwanza katika Wilaya
hiyo na kwamba ni lazima kila mwananchi ajenge utamaduni wa kupenda bidhaa
zinazozalishwa hapa nchini na kuwataka kuondokana na dhana ya kuona bidhaa
zinazotoka nje ndio bora zaidi.
“ Ukienda
kwenye nchi za wenzetu hasa zilizoendelea, wao wanathamini kwanza cha kwao, cha
mwingine badae, nasisi tukifikia hatua hiyo tutafanikiwa sana, lakini
tutafikaje hapo ni la zima kuanzia sasa tuamke tuanze kupenda vya kwetu”
amesema Mhe. Chongolo.
Mhe.
Chongolo ameongeza kuwa uwepo wa maonesho hayo utaongeza tija na mipango
madhubuti ya kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu sambamba na kuongeza
wigo mpana wa kutangaza bidhaa hizo na wananchi kupenda kuzitumia.
“ Uwepo wenu
hapa utawezesha wale wananchi ambao wanakuja kununua bidhaa zenu , ndio
watakuwa mawakala kwa wananchi wengine ambapo na wao watapenda kuja kununua
bidhaa hizi bora na nzuri za kitanzania” ameongeza.
Kwa upande wake
Diwani wa Kata ya Kawe , Mhe. Muta Rwakatare amempongeza Mhe. Chongolo kwa
kubuni na kufanikisha kuwepo kwa maonesho hayo.
Ameongeza kuwa
kutokana na umahiri aliokuwa nao mkuu huyo wa Wilaya wa kutatua changamoto
mbalimbali za wananchi, anaamini kuwa sasa ni wakati wa wajasiriamali hao
kunufaika kwani changamoto zao pia zimefikia kikomo.
Ameongeza kuwa
Rais Dk. John Magufuli amekuwa mstari wa mbele kusisitiza uchumi wa viwanda na
kwamba hadi sasa tayari adhma hiyo imefanikiwa kwa asilimia kubwa.
Naye Mkuu wa
Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele
amesema kuwa wazo la kuwepo kwa maonesho hayo lilitolewa na Mhe. Chongolo
wakati wa maonesho ya nanenane ambapo alihitaji kuandaliwa kwa mpango kazi wa
kuwa na maonesho hayo.
Amesema kuwa
kabla ya kufanyika kwa maonesho hayo, awali yalifanyika mafunzo ya siku nne
ambayo yaliendana sambamba na maonesho ya bidhaa hizo kwa siku moja yaliyofanyika
katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Dk. Henjewele amesema kuwa maonesho hayo ya
siku nne yatafikia kilele Disemba 15 ambapo bidhaa zote za ngozi ikiwemo viatu,
mikoba, mikanda na mabegi ya shule ya wanafunzi yanapatikana hapo.
No comments:
Post a Comment