Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Patterson, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Makubusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo Desemba 13, 2019. (Picha na Faraja Ezra).
TAASISI isiyo ya kiserikali ya Girls App kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani wametoa wito kwa watoto wa jinsia ya kike kukataa dhana zilizopo katika jamii ikiwemo kuonekana tegemezi na dhaifu.
Kuna
dhana potofu iliyojengeka katika jamii nyingi za kiafrika kuwa mtoto wa
kike hawawezi chochote na kwamba kazi yao ni kuolewa , kulea Watoto,
pamoja na kufanya kazi za nyumbani.
Badala yake watumie teknolojia iliyopo ili kuondoa dhana hizo kwa kutimiza ndoto zao kwa kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 13, 2019 Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi hiyo, Wilhelm Gasper, alisema taasisi hiyo imekuwa
ikiwakusanya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za serikali nchi kwa
miezi sita lengo likiwa lengo likiwa kutafuta mawazo mbalimbali ambayo
yatakwenda kutatua changamoto zinaikabili jamii.
Alisema
wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa namna ya kutumia kompyuta
kutengeneza tofuti ya mtandao baada ya hapo mabinti hao wanabuni miradi
mbalimbali itakayoleta tija kwa jamii.
"Na
Mara nyingi tumekuwa tukiandaa mikutano inayokutanisha wadau mbali
mbali kwa ajili ya kutafuta mshindi aliyebuni miradi mizuri na kupewa
zawadi ili wasichana wengine waige mfano huo hatimaye na wao wasibweteke
bila ya kuwa wabunifu," alisema Gasper.
Naye
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Partterson aliwaasa wasichana
kutumia teknolojia iliyopo ili kukuza uchumi wao na kuamini kwamba wao
wanaweza na kwani wao ni nguzo kwa familia .
Pia
mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne shule ya Kibasila Zahara Juma
alisema wamenufaika vya kutosha kupitia kufundishwa kutumia kompyuta
kwani wameweza kutengeneza tovuti mbalimbali kupitia mitandao ya
kijamii.
" Hii kwetu ni
fursa ya kipekee kabisa kukuza uelewa wetu na kuweza kujitegemea
kiuchumi na tumekuwa tukikutana na wadau mbali mbali kupeana uzoefu ili
kutatua changamoto zinawakabili," alisema Zahara.
No comments:
Post a Comment