MBUNGE wa Nyamagana Stanslaus Mabula, anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika mashindano ya Riadha ya Taifa ya Ngorongoro Crater
'Ngorongoro Crater National Athletics Championship ' yanayotarajiwa kuanza
kutimua vumbi kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba jijini
Mwanza.
Kwa Mujibu wa Msemaji wa Shirikisho la Riadha Tanzania
(RT), Tullo Chambo, Mheshimiwa Mabula amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika
mashindano hayo.
Chambo, alisema maandalizi yanaendelea vema na mikoa
tayari imeishaanza kuwasili.
Aliitaja mikoa iliyokuwa imewasili hadi Ijumaa mchana
ni 13 ambayo ni Simiyu, Mwanza, Singida, Dodoma, Tabora, Mara, Geita, Morogoro,
Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kaskazini Pemba, Kusini Pemba.
"Tunategemea mikoa mingine itaendelea kuwasili na
kupokelewa hadi usiku tayari kwa mashindano haya, ambayo tunatarajia kuona
vipaji vipya na ushindani mkali," alisema.
Chambo alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na
maeneo ya jirani, kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment