HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 27, 2019

MSIUZE ARDHI KWA WATU BINAFSI - DKT. BASHIRU

 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deodatus Kinawilo, akiwaongoza kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bukoba.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa  Dkt. Bashiru Ali, akizungumza wakati wa ukaguzi wa hospitali ya wilaya ya Bukoba.
 

Na Lydia Lugakila, Kagera

Katibu Mkuu wa CCM Taifa  Dkt. Bashiru Ali, ameagiza viongozi wa Serikali za vijiji kuacha mara moja ugawaji na uuzaji wa  ardhi za vijiji kwa watu binafsi wenye uchu wa madaraka, wanaojilimbikiza mali badala yake  ardhi hiyo itumike kwa matumizi ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo akiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera katika  ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo iliyopo eneo la Bujuna ngoma.

Aidha Dkt. Bashiru akikagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo ametoa pongezi kwa  wananchi wa Kijiji cha Kanazi kwa kutoa ardhi kwa ajili  ya maendeleo na kuagiza viongozi wa Serikali za vijiji kuacha mara moja ugawaji na uuzaji wa  ardhi za vijiji kwa watu binafsi wenye uchu wa madaraka wanaojilimbikiza mali badala yake  itumike kwa matumizi ya Maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Katibu huyo  amesema kuwa kwa kipindi cha nyuma tatizo hilo limekuwepo ambapo wenyeviti, na watendaji wake pamoja na halmashauri ya kijiji wamekuwa wakigawa  ardhi kwa watu binafsi  wenye lengo kujilimbikizia mali kuliko kuwekeza katika masuala ya maendele.

‘’Natoa maelekezo  kwa wanaogawa ardhi ya kijiji hawana mamlaka hayo ardhi ya kijiji hata kama ni hatua moja igawiwe kisheria na ni lazima mkutano mkuu wa kijiji uhusishe watu wenye umri wa miaka 18 wanaoishi eneo husika  wawepo wasajiliwe kwamba wameudhulia na muhtasali uwepo hapo ndo ardhi ya kijiji itaruhusiwa kugawanywa’’ alisema Katibu huyo. 

Amesema Wenyeviti wa vijiji waliochaguliwa hivi karibuni wanapaswa kusimamia sheria za ardhi na kuwa ardhi inabidi  igawiwe na mkutano mkuu wa kijiji na sio mwenyekiti wa kijiji.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya  mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Solomon Kimilike amesema mradi huo umeanza  januari 26, 2019 na umeghalimu Shilingi milioni 1.5 huku akitaja mradi huo kukumbwa na changamoto ya baadhi ya mafundi jamii waliopewa kazi ya ujenzi kuiba baadhi ya vifaa vya ujenzi ikiwemo chokaa pamoja na Masinki.

Akijibu taarifa hiyo ya Mkurugenzi Dkt Bashiru  amewaagiza wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha  miradi yote inakotekelezwa hakuna udokozi.

 Hata hivyo kwa upande wake Harouna Rweyongeza Swarehe ambaye ni mwananchi  kijijini hapo amewapongeza wananchi waliojitolea ardhi  kwa ajili ya maendeleo na kuongeza kuwa uwepo wa hospitali hiyo umesaidia pakubwa kwani kwa muda wamekuwa wakifuata  huduma ya matibabu umbali wa kilometa 20 kutoka maeneo hayo  na kuifuata hospitali ya  rufaa ya mkoa wa Kagera kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment

Pages