Naibu
Waziri wa Maji, Juma Aweso, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya
kuangalia chanzo cha maji cha Milima ya
Ulugulu katika eneo la Hululu ambapo mitambo itajengwa kwa ajili ya
kusambaza maji katika mkoa wa Morogoro.
Mhandisi
wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana na
umuhimu chanzo cha maji cha uhakika kwa
mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya
Naibu Waziri wa Maji Juma Oweso ya
kwenda kuangalia chanzo hicho cha maji.
Naibu
Waziri wa Maji, Juma Aweso, akipumuzika na
viongozi mbalimbali wakati kupanda mlima wa kufikia chanzo cha maji katika eneo
Hululu.
Sehemu ya
chanzo ambapo mtambo utajengwa kwa ajili ya maji katika mkoa wa Morogoro.
Na Mwandishi Wetu
MKOA wa
Morogoro hivi karibuni itaondokana na tatizo
la maji kutokana na kupata chanzo cha uhakika kutoka milima ya Ulugulu
katika eneo la Hululu ambapo bwawa la Mindu litatumika kama ziada ya Maji.
Chanzo cha
maji hicho kimefikiwa na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso wakati alipokwenda kuangalia chanzo
hizo na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu
pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira (Moruwasa).
Katika ziara
ya Naibu Waziri Oweso aliwaagiza na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira
(Moruwasa) kuandika andiko kwa kina ili kuwekeza miundombinu katika chanzo cha
maji cha milima Ulugulu katika eneo la Hululu.
Viongozi wa
eneo la chanzo cha maji walieleza kuwa Naibu wa Waziri huyo ni kiongozi wa
kwanza kufika eneo la chanzo cha maji tangu dunia iiumbwe na kudai kuwa
serikali ya awamu ya Tano ina udhubutu wa viongozi katika utendaji wa
kuhakikisa wananchi wa Mkoa wa Morogoro wanaondokana na tatizo la maji.
Naibu Waziri Aweso amesema kuwa kutokana na chanzo
cha maji hayo kuwepo kwa muda wote kulikuwa hakuna sababu ya kutumia Bwawa
kwani mabwawa huwekwa sehemu ambayo ni
kame hivyo mkoa wa Morogoro si Kame kwa kuwa na chanzo cha maji
kinachotegemea bwawa.
Amesema kuwa
chanzo hicho cha maji katika milima ya Ulugulu ni kufikisha Morogoro ni jirani
ukilinganisha na mradi wa maji wa Ziwa Victoria kutolewa mwanza na kwenda
katika mikoa mbalimbali ambayo ilikuwa na ukame wa maji na hawakujua watapata
katika chanzo kipi.
Nae Afisa wa
Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi
Simon Ngonyani alimweleza kuwa chanzo hicho kinatokana na utunzwaji wa
mazingira na kutaka wananchi waendelee kulinda vyanzo vya maji.
Ngonyani
amesema kuwa kuna miradi mbalimbali ya miundombinu katika Mkoa wa Morogoro
lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na kwenda kwa kasi katika
ujenzi wa viwanda ambavyo kuendelea kwake kunatokana na upatikanaji wa maji.
Mhandisi
Ngonyani amesema kuwa wanapokea maagizo ya Naibu Waziri Juma Aweso na kuahidi watafanyia kazi kwa
kuandika andiko la mradi kwa kushirikiana na Moruwasa ikiwa chanzo hicho kuanza
kufanyiwa kazi.
“Ninaamini
chanzo hiki kitakuwa mkombozi kwa wananchi wa
Mkoa wa Morogoro na kuwa historia
kutegemea bwawa kwa mkoa wenye vyanzo vya maji Lukuki hivyo bonde litaendelea kuhakikisga vyanzo
vya maji vinalindwa vizazi kwa vizazi”amesma Ngonyani.
Mkuu wa
Wilaya ya Mvomero Mwalimu Mohamed
Utaly amesema kuwa chanzo cha maji hicho kwa Mkoa wa Morogoro kwa serikali ya
awamu chanzo cha maji kitajengwa.
No comments:
Post a Comment