Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) amekutana, kufanya mazungumzo na kupokea nakala za Hati ya Utambulisho
ya Balozi Mteule wa Algeria Mhe. Ahmed
Djellal pamoja na Balozi Mteule wa Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess.
Prof.
Kabudi amekutana na mabalozi hao wateule leo jijini Dar es Salaam ambapo pamoja
na mambo mengine, kabla ya kukabidhiwa nakala za hati za utambulisho kukoka kwa
mabalozi hao, Prof. Kabudi amefanyaa mazungumzo na Mabalozi wateule ambapo mazungumzo
hayo yaliyolenga kuimarisha uhusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria pamoja Shirikisho la Ujerumani.
Waziri Kabudi alimweleza Balozi mteule wa Algeria nchini
Tanzania kuwa Tanzania na Algeria zimeendelea kuwa na uhusiano mzuri na wa
kihistoria tangu miaka ya 1960 wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika
dhidi ya ukoloni…"Misingi ya uhusiano wa Tanzania na Algeria ulijengwa na
Waasisi wa Mataifa haya mawili, Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Ahmed Ben
Bella wa Algeria," Amesema Prof. Kabudi
Waziri Kabudi ameongeza kuwa, Algeria imeendelea kuwa na
Ubalozi wake hapa nchini Tanzania tangu mwaka 1964 ikiwa ni miongoni mwa nchi
za mwanzo kabisa kufungua ubalozi hapa nchini. Mwaka 1981 nchi hizi mbili
zilianzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ambayo imechangia
kuimarisha na kukuza ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo diplomasia,
ulinzi, elimu, madini, nishati na michezo.
Kwa upande
wake Balozi mteule wa Algeria Mhe. Balozi Ahmed Djellal ameahidi kuwa Serikali
ya Algeria itaendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania hususani
diplomasia, kukuza na kuimarisha biashara, uwekezaji na utalii.
"Mimi
Balozi Mteule nitashughulikia na kuhakikisha kwamba uwekezaji na biashara
unaofanywa kati ya Algeria na Tanzania unakuwa wa manufaa kwa pande zote mbili
lengo likiwa ni kukuza sekta ya biashara hapa Tanzania" Amesema Mhe.
Balozi Djellal.
Katika tukio jingine, Prof. Kabudi amepokea nakala za Hati
ya Utambulisho za Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani hapa nchini, Mhe.
Balozi Regine Hess ambaye amemweleza Waziri Kabudi kuwa uhusiano wa
kidiplomasia baina ya Tanzania na Ujerumani ni mzuri na kuongeza kuwa jukumu
lake kubwa kwa sasa ni kuendeleza uhusiano huo.
Balozi Regine Hess ameyasema hayo wakati akikabidhi nakala
za Hati ya Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb).
Balozi
Regine Hess amesema kuwa mbali na uhusiano wa
kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani, ushirikiano mzuri uliopo wa
uwekejzaji, biashara, utalii na elimu utaendelea kuimarika na kutoa zaidi fursa
za maendeleo kwa Tanzania.
"Kuna baadhi ya wawekezaji kutoka Ujerumaani ambao
wameshaonesha nia ya kutaka kuwekeza Tanzania, hivyo nitawasiliana nao na
kuweza kujua wamefikia wapi kwani Tanzania ina sifa nzuri. Jukumu langu nikiwa
Balozi hapa ni kukuza na kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya
Ujerumani na Tanzania, hivyo nitajitahidhi niwezavyo kufanikisha jukumu
hilo," Amesema Balozi Hess.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Balozi mteule wa
Algeria nchini Tanzania Mhe. Balozi Ahmed Djellal kabla ya kuwasilisha nakala ya
Hati ya Utambulisho. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam.
Balozi mteule wa Algeria nchini Tanzania Mhe.
Balozi Ahmed Djellal akimkabidhi nakala ya Hati ya Utambulisho Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkaribisha Balozi Mteule wa
Shirikisho la Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess alipowasili katika Ofisi ndogo
za Wizara jijini Dar es Salaam kuwasilisha nakala ya Hati ya Utambulisho kwa
mhe. waziri.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Balozi Mteule wa
Shirikisho la Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess kabla ya kuwasilisha nakala ya Hati
ya Utambulisho. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi Mteule wa
Shirikisho la Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess kabla ya kuwasilisha nakala ya Hati
ya Utambulisho. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment