Mhifadhi kitengo cha ujirani mwema Zabron Mtwelve akizungumza na waandishi wa habari wa mikoa ya nyanda za juu kusini waliofanya ziara ya katika hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa lengo la kujifunza maswala ya utalii.
Na Fredy Mgunda, Serengeti
Hali ya umasikini ya
wananchi wa wanaoizunguka hifadhi ya taifa ya Serengeti ndio ilikuwa chanzo cha
wananchi kujihusisha na ujangili wa wanyama pori waliopo katika hifadhi hiyo
kwa kiasi kikuwa kwa kuwa walikuwa hawana shughuli za kuwaingizia kipato.
Akizungumza na waandishi wa habari wa mikoa ya
nyanda za juu kusini waliofanya ziara ya katika hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa lengo la kujifunza
maswala ya utalii,mhifadhi kitengo cha ujirani mwema Zabron Mtwelve alisema
kuwa baada ya kufanya utafiti na kugundua kuwa umaskini wa mtu moja moja ni
chanzo cha vitendo vya ujangili na waliamua kuanzisha Benki ya COCOBA.
“Baada ya kubaini umaskini
wa kipato kwa wananchi wanaozunguka hifadhi ya Serengeti tulianzisha miradi ya
mbalimbali ya kiuchumi kwa lengo la kuwaokoa kiuchumi wananchi hivyo moja ya
mradi tulioanzisha ni mradi wa Benkiya hifadhi ya jamii (COCOBA) ili wananchi
waondokane na vitendo vya ujangili katika hifadhi hiyo” alisema
Mtwelve alisema mara baada
ya kutoa elimu ya Benki hiyo na kutoa elimu ya madhara ya ujangili katika
hifadhi ya Serengeti vitendo vya ujangili vimepungua kwa kiasi kikubwa kiasi
kwamba ongezeko la mnyama Tembo limekuwa kubwa hivyo kuashiria kuwa ujangili
umepungua.
“Tuligundua kuwa umasikini
mtu moja moja ni tatizo linalochangia wananchi wengi kuingia kwenye hifadhi ya Serengeti
na kufanya vitendo vya ujangili hivyo shirika kwa kutumia kitengo cha ujirani
mwema tulianzisha miradi na mmoja ya mradi huo ni huu wa COCOBA ambao unasaidia
wananchi kuinua uchumi na kuacha kutegemea ujangili katika hifadhi hiyo”
alisema Mtwelve
Mtwelve Mbali na mradi huo
wa Benki ya jamii bali kuna miradi kama ya ufugaji nyuki ambayo wamekuwa
wakiitekeleza katika wilaya za Bariadi,Bunda na Tarime kwa lengo la kuendelea
kuinua uchumi kwa wananchi na kupunguza vitendo vya ujangili kwa wanyama ambao
wapo katika hifadhi hiyo.
“Kwa sasa hifadhi ya taifa
ya Serengeti mkoani mara imefanikiwa kupunguza vitendo vya ujangili mara baada
ya kuanzisha kitengo cha ujiarani mwema kwa vijiji vyote vinavyoizunguka
hifadhi hiyo ya Serengeti” alisema Mtwelve
Kwa upande wake kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebecca Msambusi alisema kuwa
vitendo vya ujangili vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na elimu ambayo
imekuwa ikitolewa mara kwa mara kwa wananchi wote ili kuendelea kuitunza na
kuilinda hifadhi hiyo.
“Tumekuwa tukitoa elimu mara
kwa mara juu ya madhara ya vitendo vya ujangili vinavyoathiri uchumi wan chi na
kwa mwananchi moja moja na tumewaeleza faida ya uhifadhi wa wanyama pori wetu
ndio maana vitendo vya ujangili vimepungua” alisema Msambusi
Msambusi aliongeza kuwa hali
ya utalii katika wilaya ya Serengeti imekuwa na watalii wanazidi kuongezeka
kila uchwao na uchumi unakuwa kutokana na wananchi kuwa na elimu ya uhifadhi
ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment