Benki ya
CRDB leo Januari 16, 2020 imezindua rasmi huduma ya “Chanja, Lipa, Sepa” kwa maduka yote
yanayokubali malipo ya kadi ambapo wateja watakaofanya malipo kwa
TemboCardVisa na SimBankingVisa wataweza kufurahia punguzo la bei hadi
asilimia 60 kwa manunuzi ya kuanzia shilingi 30,000 katika maduka na
migahawa mbalimbali hapa nchini.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara ya Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya “Chanja, Lipa, Sepa” ya Benki ya CRDB kwa
kutumia TemboCardVisa. Kampeni hiyo ilifanyika leo
kwenye Duka la Miniso, Mlimani City, jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara na Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif ,
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum
ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ijulikanayo kama “Chanja, Lipa, Sepa”
uliofanyika leo kwenye maduka ya GSM na Miniso, yaliyopo Mlimani City,
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment