HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 13, 2020

GCLA YAJIVUNIA UBORESHAJI WA MIRADI YA MAENDELEO


Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na wanahanari (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano inayojulikana kama 'Tunaboresha Sekta ya Afya' mapema leo Jijini Dar es Salaam.


Na Faraja Ezra

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), imefanikiwa kuboresha miradi pamoja na kuweka mipango mikakati ya   utekelezaji nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jiji ni Dar es Salaaam, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, ambapo alisema Mamlaka inajivunia kutekelezaji wa  miradi mikuu minne katika  kipindi cha serikali ya awamu tano.

Aidha Dkt. alifafanua baadhi ya miradi iliyotekelezwa  kwa kiwango kikubwa ikiwamo, Uwekezaji katika miundombinu ya majengo, Ujenzi wa mifumo mbali mbali ya Tehama, Upanuzi wa huduma za kikanda na kuongeza usimamizi wa sheria  ya vina Saba ya Taifa.

Alisema katika uwekezaji wa
Sekta ya miundombinu nchini Serikali imefanikiwa kuimarisha mitambo mikubwa  9 inayochunguza mambo mbalimbali ikiwamo  uchunguzi wa vina Saba,(DNA) Viambata vya suumu, Ubora wa gesi na Madini ambayo jumla imegharimu shilingi bil. 6.5 pekee.

Hivyo alisema mitambo hiyo imesaidia kurahisisha mchakato wa upatikanaji na utoaji huduma kwa umma ili kujiridhisha na uchunguzi kwa kuzingatia sheria iliyowekwa.

Pia Upanuzi wa huduma za kisasa za kimaabara za kikanda hususani Kanda za juu kusini na Kanda za kaskazini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora nchini.

Mafumiko alieleza kuwa  Serikali kupitia Mamlaka hiyo pia imewezesha  Ujenzi wa mfumo wa  kisasa wa Kielekroniki ambao hutumika kusajili wadau pamoja na kemikali ili kudhibiti ufanisi  wa rasilimali fedha inayotumika.

" Tunaishukuru serikali kwa kutuongezea rasilimali watu ambao wameonyesha jitihada kubwa katika kufanikisha utoaji wa huduma ambapo mwaka 2019 imeajiri watumishi zaidi ya 293 katika Kanda mbalimbali," alisema Dkt Mfumiko.

Mbali na hayo, Dkt. Mfumiko alisema Mamlaka imeweka mkakati wa kuanzisha  kanzidata ya kuchunguza  vina Saba (DNA) yaTaifa ili kutambua uhalali wa  mama au baba.Hii itapunguza malalamiko dhidi ya wanafamilia.

Alisema Mamlaka pia imeweka Mipango mikakati ya kuunganisha ofisi za kanda katika kila mkoa ili kurahisisha Mawasiliano nchini pamoja na kuanzisha vyombo vya usafiri ili kukidhi viwango vya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages